IQNA

Msikiti 'wa kwanza Afrika' Wakarabatiwa Ethiopia

22:22 - October 24, 2018
Habari ID: 3471718
TEHRAN (IQNA)- Msikiti wa Al-Nejashi nchini Ethiopia, unaoaminika kuwa msikiti kwa kwanza kujengwa barani Afrika, umekarabatiwa.

Msikiti huo ambao pia unajulikana kama Negash Amedin Mesgid uko katika mji wa Wuqro yapata kilomita 790 kaskazini mwa mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa unaaminika kujengwa karne ya 7 Miladia (kati ya mwaka 23 Kabla ya Hijrah na 81 baada ya Hijrah).
Jina la msikiti huo linanasibishwa na Mfalme Nejashi aliyekuwa akitawala Ethiopia au Uhabeshi wakati maswahaba wa Bwana Mtume Muhammad SAW waliofika katika nchi kukimbia na ukandamizaji waliokuwa wamekumbana nao katika mji wa Makka.
Maswahaba hao walikimbilia hifadhi Uhabeshi kufuatia amri ya Bwana Mtume SAW aliyesema mfalme wa ardhi hiyo alikuwa muadilifu. Msikiti huo umekarabatiwa hivi karibuni kwa hisani ya Wakala wa Uratibu na Ushirikiano nchini Uturuki (TIKA).
Msikiti huo uko katika eneo pana ambalo pia linajumuisha makaburi 15 ya maswahaba wa Mtume SAW.
Imamu wa Msikiti wa Al-Nejashi Sheikh Ali Mohammad Ibrahim amewapongeza wafadhili kutoka Uturuki kwa kukarabati eneo hilo la kihistoria. Anasema msikiti huo mbali na kuwa eneo la ibada kwa Waislamu pia ni kivutio kwa watalii Wakristo.

3467057

captcha