IQNA

Washindi wa Mashindano ya Qur'ani Tunisia Watangazwa

20:36 - December 15, 2018
Habari ID: 3471772
TEHRAN (IQNA) – Washindi wa Mashindano ya 16 ya Kimataifa ya Qur'ani nchini Tunisia wametangazwa na kutunukiwa zawadi zao.

Sherehe za kuwatunuku zawadi waliofanya vizuri katika mashindano hayo zimefanyika Disemba 13 mjini Carthage ambapo mgeni wa heshima alikuwa ni Waziri wa Masuala ya Kidini Ahmed Azoum.

Katika kitengo cha kuhifadhi kikamilifu Qur'ani Tukufu mshindi alikuwa ni Mohammad Abduqadir Moaref wa Tunisia huku nafasi ya pili ikishikwa na Adam Salih wa Sudan na Mohammad Mostafa Mujtaba wa Mauritani amechukua nafasi ya tatu.. Katika kitengo cha qiraa na tajwidi mshindi alikuwa Abduljalil Bouski wa Morocco na nafasi ya pili ilishikwa kwa pamoja na Mohammad Hassan Mowahedi wa Iran na Lutfi Turhan wa Uturuki.

Mashindano ya 16 ya Kimataifa ya Qur'ani nchini Tunisia yalifanyika mjini Carthage kuanzia Disemba 8-13 na kulikuwa na washiriki kutoka nchi 31.

3772159

captcha