IQNA

Ajuza wa Miaka 75 ahifadhi Qur'ani Kikamilifu

10:43 - January 27, 2019
Habari ID: 3471820
TEHRAN (IQNA)- Ajuza mwenye umri wa miaka 75 nchini Saudi Arabia amefanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.

Ajuza wa Miaka 75 ahifadhi Qur'ani KikamilifuKwa mujibu wa taarifa, Mansiya bint Saeed bin Zafir al-Aliyani amefanikiwa kuhifadhi Qur'ani kikamilifu pamoja na kuwa hajui kusoma wala kuandika.
Imedokezwa kuwa anaishi katika kijiji cha al Bujaila katika eneo la Asir, kusinig magharibi mwa Saudi Arabia.
Bi.Mansiya amefanikiwa kuhifadhi Qur'ani kwa kusikiliza qiraa za wasomaji mashuhuri wa Qur'ani.
Aidha alihudhuria darsa za kuhifadhi Qur'ani katika kituo cha Darul Qur'an kijijini hapo.
Qur'ani Tukufu ni kitabu pekee kitakatifu ambacho waumini wanaokifuata huweza kukihifadhi kikamilifu.
Katika kila jamii ya Waislamu duniani, hupatikana watu ambao wamehifadhi Qur'ani kikamilifu.

3784331

captcha