IQNA

20:36 - April 13, 2019
News ID: 3471914
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran maalumu kwa ajili ya wanawake yamemalizika Ijumaa mjini Tehran.

Wawakilishi kutoka nchi saba ambazo ni Iraq, Afghanistan, Algeria, Tunisia, Lebanon, Iran na Indonesia walishindano katika fainali hizo na washindi wanatazamiwa kutangazwa Jumapili.

Leo Jumamosi washiriki katika mashindano hayo wametembelea Haram Takatifu ya Imam Ridha AS.

Mashidano hayo ya Qur'ani ya wanawake ni kati ya mashindano mengine ambayo yanafanyika nchini Iran.

Mbali na mashindano ya kawaida ambayo ni Mashindano ya 36 ya Qurani ya  wanaume pia kunafanyika mashindano maalumu kwa ajili ya wanawake, wanafunzi wa vyuo vya kidini, wanafunzi wa shule na walemavu wa macho ambao watashindana katika kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu.  Washiriki wa mashindano hayo ya Qur'ani wanashindana katika kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu.

Mwaka huu washiriki 184 wa mashindano ya Qur'ani kutoka nchi 84 walifanikiwa kufika katika nusu fainali ya mashindano ya mwaka huu.
Nusu fainali ya mashindano hayo ilifanyika Jumanne Aprili 9 na Jumatano Aprili 10 asubuhi kabla ya ufunguzi rasmi wa fainali alasiri ya Jumatano ambapo inatazamiwa kuwa mashindano yatamalizika Aprili 14.

3803026

Name:
Email:
* Comment: