IQNA

13:13 - April 08, 2019
News ID: 3471905
TEHRAN (IQNA) – Nchi 27 zitawakilishwa katika Mashindano ya 6 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran maalumu kwa ajili ya wanafunzi wa shule.

Hayo yamedokezwa Jumapili mjini Tehran na Mohammad Reza Mosayyebzadeh mkuu wa kamati andalizi ya mashindano hayo.

Ameongeza kuwa  mashindano hayo yatafanyika mjini Tehran kuanzia Jumatano na yatakuwa na vitengo vya wavunala na wasichana.

Mashindano ya mwaka huu yameandaliwa na Wizara ya Elimu ya Iran. Mashindano hayo ni sehemu ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran ambayo yanafanyika wiki hii mjini Tehran

Mashindano ya Kawaida ya 36 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yatafanyika sambamba na mashindano ya vitengo maalumu vya wanawake, watu wenye ulemavu wa macho, wanafunzi wa vyuo vya kidini na wanafunzi wa shule.

3801396

Name:
Email:
* Comment: