IQNA

10:58 - April 08, 2019
News ID: 3471904
TEHRAN (IQNA) – Washiriki wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wameanza kuwasili nchini.

Akizungumza na waandishi habari mjini Tehran Jumapili, Hujjatul Islam Sayyid Mustafa Husseini, mkuu wa kamati andalizi amesema washiriki 184 wa mashindano ya Qur'ani kutoka nchi 84 wamefanikiwa kufika katika nusu fainali ya mashindano ya mwaka huu.

Ameongeza kuwa nusu fainali ya mashindano hayo itafanyika Jumanne Aprili 9 na Jumatano Aprili 10 asubuhi na ufunguzi rasmi wa fainali utafanyika baadaya alasiri siku hiyo hiyo na kuendelea hadi Aprili 14

Mashindano ya Kawaida ya 36 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yatafanyika sambamba na mashindano ya vitengo maalumu vya wanawake, watu wenye ulemavu wa macho, wanafunzi wa vyuo vya kidini na wanafunzi wa shule.

Hujjatul Islam Sayyid Mustafa Husseini amesema pembizoni mwa mwashindano hayo kutakuwa na hafla kadhaa za kiutamaduni na pia maoneyesho kadhaa.

Mashindano  hayo, sawa na miaka iliyotangulia yanafanyika katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini MA hapa mjini Tehran.

Kinyume na miaka iliyopita, mwaka huu kumekuwa na raundi tatu, ambapo katika raundi ya kwanza washiriki walituma fomu za maombi ya kushiriki zikiwa zimeambatana na faili la sauti ya qiraa yao. Wale ambao walionekana kuwa na viwango stahiki, wamealikwa Iran kushiriki katika mashindano ya nusu fainali.Washiriki wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani waanza kuwasili Iran

Shirika la Wakfu la Iran huandaa mashindano ya kimatiafa ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani ya Iran kila mwaka ambapo huwa na washiriki kutoka kila kona ya dunia.

Mwaka jana kulikuwa na washiriki 370 wa kigeni waliohudhuria mashindano ya kimataifa ya Qur'ani.

3801396

Name:
Email:
* Comment: