IQNA

18:05 - June 02, 2019
News ID: 3471981
TEHRAN (IQNA)- Wanajeshi na walowezi wa Kizayuni wameuvamia na kuvunjia heshima Msikiti wa al Aqsa na matukufu mengine ya Kiislamu.

Katika tukio hilo leo Jumapili wanajeshi na walowezi wa Kizayuni wameuvamia tena Msikiti wa al Aqsa ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu na kukabiliwa na upinzani mkubwa wa Waislamu wa Palestina. 

Wanajeshi makatili wa Israel wameugeuza Msikiti wa al Aqsa kuwa kituo cha kuonyeshea ubabe wao ambapo wanaendesha kampeni kubwa ya kuangamiza utambulisho wa Kiislamu na Kikristo wa eneo hilo. 

Kwa mujibu wa baadhi ya taarifa, Wazayuni wamevamia ndani ya msikiti huo mtukufu na kufanya uharibifu wa mali za Waislamu. Kitendo hicho cha Wazayuni kimelaaniwa vikali na harakati mbali mbali za kupigania ukombozi wa Palestina.

Mwaka 2017 Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) lilitangaza rasmi kuwa Msikiti wa al Aqsa ni wa Waislamu na kwamba Mayahudi hawahusiki kivyovyote vile na msikiti huo. Mji ulipo msikiti huo una maeneo matukufu mengi ya Waislamu, Wakristo na Mayahudi.

3468659

Name:
Email:
* Comment: