IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
10:42 - June 05, 2019
News ID: 3471986
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesem siri ya kuendelea kubakia hai na kuwa na mvuto fikra za Imam Khomeini MA, inatokana na sifa maalumu ya shakhsia na tunu aliyopewa na Mwenyezi Mungu.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei  Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyasema hayo jana mjini Tehran alipohutubu katik mbele ya hadhara kubwa  katika Haram tukufu ya Imam Khomeini (MA) kwa mnasaba wa mwaka 30 wa kuaga dunia muasisi huyo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Akibainisha wigo na vipengee vya 'njia na mantiki ya mapambano au muqawama na kusimama kidete' kama somo kubwa la Imam Khomeini MA kwa ajli ya mataifa na viongozi alisema kuwa, fikra na njia hiyo zinaendelea kuyavutia  kila siku mataifa mbalimbali. Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema kuwa ushiriki mkubwa wa wananchi katika kumbukumbu za mwaka wa 30 za kufariki dunia Imam Ruhullah Khomeini MA na pia ushiriki wao katika Siku ya Kimataifa ya Quds, unaonyesha wazi kuendelea kuvutia fikra za Mwasisi huyo wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza kwamba Siku ya Quds iliadhimishwa katika zaidi ya nchi 100 za dunia. Amezidi kubainisha kwamba jambo hilo linabainisha kuwa miaka 40 tangu shakhsia huyo alipoaitangaza siku hiyo, hadi leo imeendelea kuwa kivutio na kupenya zaidi kiasi kwamba mataifa mbalimbali yanaendelea na harakati hiyo.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, sababu ya mataifa kupokea njia ya Imam Khomeini, yaani muqawama inatokana na dhati ya njia hiyo kuvutia na amebainisha kwamba katika mwenendo huo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijayatwisha mataifa fikra hiyo kama ambavyo pia hata kufanyika maandamano au maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds ya mwaka huu katika zaidi ya nchi 100 pia kulitokana na chaguo la watu wa mataifa hayo wenyewe. Kiongozi Muadhamu ameuelezea 'Muqawama' kuwa ni neno shirikishi ambalo linakubaliwa na watu wa mataifa yote ya Asia Magharibi na amesema kuwa, hivi sasa baadhi hawana uthubutu wa kuingia katika ulingo, ingawa wengi wao tayari wako katika ulingo huo. Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameuzungumzia pia mrengo wa muqawama hii leo kuwa unazidi kuwa wenye nguvu na kuongeza kwamba, kushindwa Wamarekani nchini Lebanon, Iraq, Syria na Palestina ni dhihirisho la uwezo wa muqawama huo. Aidha akiashiria takwimu rasmi zinazoonyesha kusambaratika uchumi wa Marekani na kupungua kwa ajabu taathira ya Washington katika uchumi wa dunia amesema kuwa, katika uga wa kisiasa pia uwezo wa Marekani umesambaratika ambapo kuchaguliwa mtu mwenye sifa kama za Donald Trump, ni ishara ya wazi na nzuri ya kusambaratika siasa za Marekani.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kwamba kukabidhi mustakbali wa zaidi ya jamii ya watu milioni 300 wa Marekani katika mikono ya mtu ambaye mlingano wake wa kifikra, saikolojia na kiakhlaqi haueleweki na ni wenye kutia mashaka, ni ishara ya wazi ya kusambaratika Marekani kisiasa na kiakhlaqi. Ayatullah Khamenei amebainisha kuwa moja ya dalili nyingine za kuporomoka kiakhlaqi serikali ya Marekani ni uungaji mkono wa serikali ya nchi hiyo kwa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina na kadhalika uungaji mkono wake kwa jinai za mataifa kadhaa yanayoishambulia Yemen na mauaji dhidi ya raia wasio na hatia wa nchi hiyo ya Kiarabu na amefafanua kuwa, katika uga wa kijamii pia Marekani inakabiliwa na matatizo mengi kikiwemo kiwango cha juu cha mauaji, jinai, njaa kali, matumizi ya dawa za kulevya na mihadarati na ukatili. Amesema kuwa katika mazingira hayo Rais wa Marekani anajionyesha kuwaonea huruma watu wa Iran, lakini anatakiwa kuambiwa kuwa kama anaweza basi na kwanya atatue matatizo yanayomkumba.

http://iqna.ir/fa/news/3816878

Name:
Email:
* Comment: