IQNA

14:22 - June 10, 2019
News ID: 3471994
TEHRAN (IQNA) – Washindi wa mashindano ya Qur'ani ambayo yaliandaliwa kwa pamoja na Radio Bilal na Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Uganda wametangazwa katika sherehe iliyofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kampala.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, sherehe za kuwatunuku zawadi ziliandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Uganda na kuhudhuriwa na mufti wa nchi hiyo Sheikh Sha'ban Ramadhan Mubaje, mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Uganda Mohammad Reza Ghezelsofla, maimamu na viongozi wengine wa kidini nchini humo.

Mashindano hayo yalifanyika katika kategoria za kuhifadhi Qur'ani kikamilifu, kuhifadhi juzuu 15 na kuhifadhi juzuu 10 pamoja na qiraa.

Mashidano hayo yamefanika kwa muda wa siku 20 na kujumuisha wanafunzi 120 wa shule za msingi na upili katika studo za Radio Bilal ambapo washiriki 15 wametunukiwa zawadi.

Akihutubu katika sherehe za kuwatunuku zawadi washindi, Mufti Mkuu wa Uganda Sheikh Ramadhani Mubajje ameshukuru Kituo cha Utamaduni cha Iran kwa kufadhili mashindano hayo ya Qur'ani na pia kwa kuunga mkono harakati za Baraza Kuu la Waislamu Uganda. Aidha ametoa wito kwa Waislamu Uganda kudumisha umoja, amani na udugu miongoni mwao huku akiwataka wajiepushe na mifarakano.

Kwa upande wake, mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha Iran amesema lengo la kufanyika mashindano hayo ya kuhifadhi Qur'ani ni kuwahimiza Waislamu kutekeleza mafundisho ya kitabu hicho kitukufu.

3817969

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: