IQNA

10:17 - July 09, 2019
News ID: 3472036
TEHRAN (IQNA) - Mwana wa Sheikh Ibrahim Zakzaky Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria ametahadharisha kupitia ujumbe aliotoa kwamba hali ya kimwili ya baba yake ni mbaya sana. Amesema karibu njia zote zimeshindikana kwa ajili ya kunusuru maisha yake.

Muhammad Ibrahim Zakzaky ameeleza kuwa kuna mada nyingi za sumu ya risasi na cadmium kwenye damu ya baba yake na kwamba serikali ya Nigeria haijachukua hatua yoyote ya kumfikisha hospitali Sheikh Zakzaky ili alazwe kwa ajili ya matibabu. Hali ya kiongozi huyo wa Waislamu hivi sasa ni mbaya ikiwa imepita miaka mitatu na nusu tangu kiongozi huyo wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria afungwe jela kinyume sheria na kutoachiwa huru licha mahakama nchini humo kuamuru aachiwe huru.
Chunguzi mpya za kitiba zimethibitisha kuwa katika damu ya Sheikh Zakzaky kuna mada za sumu ya risasi na cadmium; jambo linaloonyesha kuwa sumu hiyo alipewa akiwa jela. Harakati ya Kiislamu ya Nigeria kwa mara nyingine tena imetaka kuachiwa huru Sheikh Zakzaky na mkewe kufuatia kuzidi kuwa mbaya hali ya kiafya na kiongozi huyo wa Waislamu na mkewe. Hata hivyo Mahakama Kuu katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria haijakubali kuwaachia huru watu hao tajwa.
Wakati huo huo, wanachama kadhaa wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria wamemuonya rais wa nchi hiyo kuhusu hali mbaya ya Kiafya ya kiongozi wa harakati hiyo, Sheikh Ibrahim Zakzaky.
Kwa mujibu wa Press TV, onyo hilo limetolewa leo na wanachama hao wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria wakisema kuwa, kama baya lolote litamtokea Sheikh Ibrahim Zakzaky basi lawama zote zitakwenda kwa Rais Muhammadu Buhari.
Harakati ya Kiislamu ya Nigeria inashinikiza kuachiliwa huru Sheikh Zakzaky na mkewe hasa kutokana na Mahakama Kuu ya nchi hiyo kutoa amri ya kuachiliwa huru.
Itakumbukwa kuwa Sheikh Ibrahim Zakzaky akiwa na mke wake walitekwa nyara na Jeshi la Nigeria mwezi Disemba mwaka 2015 wakati askari walipovamia kituo chake cha kidini huko katika mji wa Zaria jimboni Kaduna. Tokea wakati huo Sheikh Zakzaky na mkewe wamekuwa wakizuiliwa katika mojawapo ya vituo vya kijeshi vya nchi hiyo bila kufunguliwa mashtaka.
Uvamizi huo ulijiri baada ya Jeshi la Nigeria kudai kuwa wafuasi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria walikuwa na njama ya kutaka kumuua mkuu wa jeshi hilo, madai ambayo yalikanushwa vikali na wafuasi wa harakati hiyo.Inakadiriwa kuwa Waislamu 1000 wasio na hatia waliuawa katika tukio hilo.

3468898/

Name:
Email:
* Comment: