IQNA

23:16 - July 19, 2019
News ID: 3472048
TEHRAN (IQNA) - Wahalifu wameuhujumu msikiti na kuvunjia heshima nakala za Qur'ani Tukufu maghairbi mwa Ujerumani.

Kwa mujibu wa taarifa, hujuma hiyo imejiri Jumanne katika msikiti mjini Munster maghairbi mwa Ujerumani ambapo wahalifu walichanachana nakala za Qur'ani Tukufu katika Msikiti wa Barbaros ambao unasimamiwa na Jumuiya ya Kiislamu na Masuala ya Kidini wa Uturuki (DITIB).
Kwa mujibu wa afisa mwandamizi wa DITIB, Sebahattin Cigdem amesema uchunguzi umeanza kuhusu hujuma hiyo ambayo imetathminiwa kuwa ni kutendo cha chuku dhidi ya Uislamu au Islampohobia. Katika kipindi cha siku 10 zilizopita nchini Ujerumani, misikiti sita inayosimamiwa na DITIB imehujumiwa pamoja na msikiti mwingine uanosimamiwa na jumuiya moja ya Kiarabu.
Ujerumani imeshuhudia ongezeko kubwa la chuki dhidi ya Uislamu na pia chuki dhidi ya wahajiri wa kigeni kufuatia kuimarika vyama vya kibaguzi vya mrengo wa kulia. Vyama hivyo vya kibaguzi vya mrengo wa kulia vimepata umaarufu kutokana na hofu itoanayo na ongezeko la wakimbizi na ugaidi.
Mwaka jana polisi nchini Ujerumani waliripoti vitendo 813 vya chuki dhidi ya Waislamu ambapo Waislamu 54 walijeruhiwa katika mashambulizi ambayo aghalabu yalitekelezwa na wabaguzi wenye misimamo ya kufurutu ada.
Ujerumani ni nchi yenye idadi ya watu zaidi ya milioni 81 na ina Waislamu takribani milioni tano na hivyo kuifanya nchi ya pili kwa idadi ya Waislamu Ulaya Magharibi baada ya Ufaransa.

3468987

Name:
Email:
* Comment: