IQNA

16:17 - August 26, 2019
News ID: 3472101
TEHRAN (IQNA) - Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amehutubu Jumapili usiku mjini Beirut kwa munasaba wa kukombolewa eneo la Juroud Arsal kutoka mikononi mwa magaidi, na katika hotuba yake ametoa radiamali kali kuhusu mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya mhimili wa muqawama na kusema jeshi la Israel lisubiri jibu wakati wowote ule kuanzia Jumatatu usiku.

Maeneo ya Juroud Arsal na Qalamoun magharibi yalilikombolewa kutoka kwa magaidi wakufurishaji mnamo Julai 2017. Hizbullah ilishirikiana na majeshi ya Lebanon na Syria katika kukomboa maeneo hayo mawili.

Baada ya kukombolewa maeneo hayo, Lebanon haikishuhudia tena mashambulizi ya kigaidi na magaidi hawakuwa tena na maficho nchini humo.

Kwa msingi huo kukombolewa maeneo hayo kulikuwa ni tukio muhiimu ndio sababu Sayyed Hassan Nasrallah akaungumza kwa mnasaba huo.

Lakini sehemu muhimu ya hotuba ya Katibu Mkuu wa Hizbullha ilihusu hujuma za hivi karibuni za Israel dhidi ya mhimili wa muqawama ikiwemo mashambulizi dhidi ya Lebanon. 

Mapema Jumapili,  ndege mbili zisizo na rubani (drone) zilikiuka anga ya Lebanon na kuanguka eneo  la kusini mwa Beirut.

Nukta muhimu katika hotuba ya Sayyid Nasrallah ilikuwa ni hii kuwa, si tu kuwa hakupuuza shambulizi hilo la Israel bali amesema kwa yakini shambulizi hilo halitabakia bila jibu. Jeshi la Israel sasa linapaswa kusibiri jibu kali la Harakati ya Hizbullah ya Lebanon. Ukweli ni kuwa kubakia kimya mbele ya uchokozi wa utawala wa Kizayuni ni jambo ambalo litapelekea utawala wa Kizayuni ukariri mashambulizi yake hayo na kuuonyesha mhimili wa muqawama kuwa ni dhaifu.

Kwa msingi huo, Sayyid Hassan Nasrallah ametoa onyo la wazi kwa Israel na kusema: "Sisi katika muqawama wa Lebanon tuko tayari kugharamika lolote ili kuhakikisha mwenendo huu haukaririwi tena. Zimefika ukingoni zile zama ambazo ndege za Israel zilikuwa zinaingia anga ya Lebanon na kushambulia maeneo kadhaa na kubakia katika usalama."

Nukta nyingine katika hotuba ya Sayyid Hassan Nasrallah ni kuwa kuna ufungamano katika mashamabulizi ya hivi karibuni ya Israel katika ardhi za Iraq, Syria na Lebanon.

Kwa maneneo mengine, ni kuwa, ingawa Katibu Mkuu wa Hizbullah ametangaza kuwa watajibu shambulizi la Israel dhidi ya mamlaka ya kujitawala Lebanon, lakini amediriki kwa njia iliyosahihi mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel katika eneo na kubaini kuwa hakutana tafauti baina ya hujuma za Israel huko Syria, Lebanon na Iraq. Amesema mashambulizi hayo ni katika fremu ya mpango maalumu ambao unatekelezwa na utawala wa Kizayuni. Katika hotuba yake Sayyid Nasrallah pia ametupilia mbali madai ya Israel kuwa eneo ambalo wamelenga Syria yalikuwa lilikuwa ni kituo cha Wairani.

Nukta ya tatu ni kuwa, Sayyid Hassan Nasrallah anaamini kuwa, baada ya vita vya mwaka 2006, Lebanon ilipata uhuru wa kweli na heshima na hivi sasa inasisitiza kulinda na kuimarisha hali hiyo. Kwa msingi huo, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa: "Sisi tuko tayari kukumbwa na baa la njaa lakini tuishi kwa heshima na katu hatutaruhusu heshima yetu ipate pigo au itishiwe."

Nukta ya nne ya hotuba ya Katibu Mkuu wa Hizbullah Jumapili usiku ni kuwa,  Waziri Mkuu wa Utawala wa Kizayuni Benjamin Netanyahu anafuatilia malengo yake ya kiuchaguzi katika kushambulia mhimili wa muqawama. Hii inamaanisha kuwa mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel huko Iraq, Syria na Lebanon yanakusudia kubadilisha mitazamo ya fikra za umma katika utawala wa Kizayuni. Kama alivyosoma Sayyed Hassan Nasrallah, mashambulizi hayo yanatokana na hofu aliyonayo Netanyahu kuhusu uchaguzi wa Septemba.

3469247

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: