IQNA

Baada ya onyo kali la Sayyed Hassan Nasrallah
11:17 - September 02, 2019
News ID: 3472109
TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imeangamiza moja ya zana za kijeshi za Israel katika barabara ya al Thakna katika mji wa mpakani wa Israel wa Avivim na kumuua kamanda wa kikosi kimoja wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel huko kaskazini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu katika oparesheni iliyotekelezwa na harakati ya Hizbullah.

Harakati ya Hizbullah imetoa taarifa ikieleza kuwa kundi la mashahidi Hassan Zebib na Yassir Tahir ndilo lililotekeleza oparesheni hiyo Jumapili Alasiri. Televisheni ya al Aalam pia imeripoti kuwa jeshi la Israel limewaagiza wakazi wa maeneo ya mpakani na Lebanon  kusalia majumbani. Televisheni ya al Jazeera pia imevinukuu vyombo vya habari vya jeshi la Israel na kutangaza kuwa: Jeshi hilo limewataka wakazi wa maeneo ya kandokando na mipaka ya Lebanon yaliyoko katika  umbali wa kilomita nne.

Ripoti zilizotufikia zinasema kuwa, Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Israel ameelekea katika Wizara ya Vita ya utawala huo kwa ajili ya kikao cha dharura pamoja na wakuu wa majeshi na wa idara za intelijinsia za utawala ili kufuatilia hali ya mambo inayoendelea sasa katika mipaka ya Lebanon.

Vyombo vya habari vya Lebanon aidha vimetangaza kuwa jeshi la Israel limetumia risasi zenye mada za fosiforasi kushambulia maeneo ya kandokando mwa Maroun  al Ras kusini mwa Lebanon.

Siku moja kabla ya oparesheni hiyo, Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayyid Hassan Nasrallah, akizungumza kwa munasaba wa kuanza Mwezi wa Muharram, alisema kwa kutumia mbinu maalumu na kulingana na irada yake na kwa namna utakavyotaka, Hizbullah itachagua wakati, mahali na mazingira mwafaka kwa ajili ya kutoa jibu kwa uvamizi uliofanywa na Israel.

Sayyid Hassan Nasrallah alibainisha kuwa, Hizbullah inacho kiwango cha kutosha cha makombora yanayolenga shabaha kwa umakini na kusisitiza kwamba, muqawama uko tayari kwa makabiliano yoyote yale madogo au makubwa na adui Israel.

Katika muda wa wiki moja iliyopita, ndege zisizo na rubani za utawala wa Kizayuni zimekiuka mara tatu mipaka ya anga ya Lebanon.

Na hii ni pamoja na kwamba, baada ya kumalizika vita vya siku 33 vya mwaka 2006 vilivyoanzishwa na Israel dhidi ya Lebanon, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio nambari 1701, ambalo liliutahadharisha utawala huo wa Kizayuni na uchukuaji hatua zozote za kiuadui dhidi ya Lebanon; lakini utawala huo limelipuuza azimio hilo na kuendelea kukiuka kila mara mipaka ya anga, ardhini na baharini ya nchi hiyo.

3469304

Name:
Email:
* Comment: