IQNA

Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon
13:06 - September 21, 2019
News ID: 3472141
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amekosoa msimamo wa baadhi ya nchi na asasi kuhusu shambulizi la ulipizaji kisasi la Jeshi la Yemen dhidi ya vituo vya kusafisha amfut aya petroli nchini Saudi Arabia na kusema, misimamo hiyo inaonyesha kuwa mafuta ya petroli yana thamani zaidi ya damu ya mwanadamu.

Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameyasema hayo Ijumaa alasiri mjini Beirut kwa munasaba wa kumbukumbu ya kuaga dunia Sheikh Hussein Kourani, mmoja wa waasisi wa Baraza la Kistratijia la Hizbullah. Katika hotuba yake Sayyed Hassan Nasrallah amesema Hizbullah iliasisiwa kufuatia jitihada za  maulmaa, wahadhiri na mujahidina na miongoni mwao alikuwemo Sheikh Kourani.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amewashauri watawala wa Saudi Arabia wakomesha mashambulizi ya umwagaji damu nchini Yemen kwa maslahi ya taifa lao.

Ameendelea kubainisha kuwa, "Saudia inashauriwa isitishe kusitisha mashambulizi dhidi ya wananchi wa Yemen badala ya kununua mfumo mpya wa ulinzi wa anga."

Amesema mifumo hiyo ya ulinzi haiwezi kuikinga na kuifanya salama Saudia kutokana na mashambulizi ya ndege siziso na rubani ya Wayemen.

Hali kadhalika Sayyid Hassan Nasrullah amewataka viongozi wa Riyadh kutafuta muafaka na Iran, akisisitiza kuwa shambulizi lolote dhidi ya Iran haitakuwa kwa maslahi ya Saudia au Imarati.

Siku chache zilizopita, Katibu Mkuu wa Harakati ya muqawama wa Kiislamu ya Lebanon (Hizbullah) alisema vita vyovyote vile dhidi ya Iran vitakuwa na maana ya kuangamizwa na kufutwa katika uso wa dunia, dola pandikizi la Israel.

Kiongozi wa Hizbullah amesisitiza kuwa, harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Lebanon inashikamana na msimamo wake wa kukabiliana na tishio la aina yoyote kutoka kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.

3469446/

Name:
Email:
* Comment: