IQNA

Kiongozi wa Hizbullah
11:14 - December 14, 2019
News ID: 3472275
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema Marekani inafanya juu chini kutaka kuonesha kuwa Hizbullah ni tishio kwa Lebanon, na kwamba njama zote hizo zinafanyika kwa ajili ya kupigania maslahi yake na ya utawala wa Kizayuni.

Sayyid Hassan Nasrullah alisema katika hotuba yake aliyoitoa jana Ijumaa katika televisehni ya Al Manar na kusema "Marekani haishughulishwi wala kuguswa na maslahi ya taifa la Lebanon. Washington inatoa mamilioni ya dola kwa ajili ya kuchafua taswira ya Hizbullah, lakini bila shaka njama hizo zitagonga mwamba."

Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema njama ghalati za Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo zimekuwa zikigonga mwamba kutokana na uwepo na kusimama kidete harakati hiyo ya muqawama. Aidha ameongeza kuwa, "Hizbullah ni tishio kubwa kwa njama za Marekani na Israel katika eneo la Asia Magharibi."

Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, Marekani na utawala haramu wa Israel zimekuwa zikibadilisha matamshi yanayotolewa na viongozi wa Iran, ili kulichochea taifa la Lebanon dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ina uwezo wa kujihami na kujilinda, sambamba na kujibu mashambulizi tarajiwa ya Marekani na Israel.

Ameongeza kuwa, harakati Hizbullah imejiandaa kwa ajili ya kuusambaratisha kikamilifu utawala wa Kizayuni wa Israel, iwapo Tel Aviv itathubutu kuanzisha hujuma yoyote dhidi ya Iran ya Kiislamu.

3470097

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: