IQNA

13:24 - October 05, 2019
News ID: 3472159
TEHRAN (IQNA)- Shule ya upili imefunugliwa Misri na kupewa jina la mcheza soka mashuhuri wa nchi hiyo, Mohammad Salah.

Kwa mujibu wa taarifa, Shule ya Upili ya Ufundi wa Kijeshi ya Mohammad Salah imefunguliwa katika karibu na mji wa Bassioun, mkoani Gharbia nchini Misri. Shule hiyo na ya kwanza ya aina yake mjini humo na ni kati ya shule bora 27 za kiufundi nchini Misri. Shule hiyo, imepewa jina la nyota huyo wa Misri ambaye ni mchezaji shupavu wa Timu ya Ligi Kuu ya Uingereza ya Liverpool na iko katika kijiji cha Nagrig alikozaliwa Salah yapata kilimita 100 kutoka Cairo.

Imedokezwa kuwa shule kwanza imefanyiwa ukarabati uliogharimu dola za Kimarekani 770,000 na ina wanafunzi 2,715. Ukarabatia huo umefadhiliwa kikamilifu na Salah ambaye pia amejenga uwanja wa kisasa wa mpira shuleni hapo.

"Mohammad Salah ni fahari kwa mchezo wa soka Misri na kimataifa," amesema Mohamed Hassan, mwalimu katika shule hiyo. Ameongeza kuwa, "ni fahari yangu kuwa alikuwa miongoni mwa wanafunzi wangu miaka 10 iliyopita. Allah Ambariki." Aliyekuwa gavana wa ene hilo Daif Saqr aliamua kuipa shule hiyo jina la Salah baada ya kufunga bao ambalo liliipelekea Misri katika Kombe la Dunia mwaka 2018.

Mchezaji huyu ni Mohammad Salah ambaye pia ni maarufu kwama 'Mfalme wa Misri' ambaye ametajwa kuwa miongoni mwa wachezaji bora katika Ligi Kuu ya Uingereza hivi sasa na ana wafuasi wengi ambao wanavutiwa na kipaji chake na pia kufungamana kwake na mafundisho ya Kiislamu. Idadi kubwa ya mashabiki wa Liverpool wameweza kuvutiwa na Uislamu kutokana na maadili bora ya Salah ambaye ametajw akuwa mfano wa kuigwa.

3847274

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: