IQNA

21:49 - November 26, 2019
News ID: 3472231
TEHRAN (IQNA) –Jeshi la kujitolea la wananchi nchini Iran maarufu kama Basiji limezindua chekechea 620 mpya za Qur’ani Tukufu kote nchini.

Chekechea hizo ambazo zinajikita katika kutoa mafunzo ya Qur’ani na kuhimiza mafundisho kwa mujibu wa Qur’ani zimezinduliwa kwa munasaba wa Wiki ya Basiji nchini Irna.

Kwa uzinduzi huo, hivi sasa kuna chekechea 3,600 za Qur’ani kote Iran zinazosimamiwa na Taasisi ya Basiji.

Inafaa kuashiria hapa kuwa Novemba 26 mwaka 1979, jeshi la kujitolea la wananchi (Basiji) liliundwa kutokana na amri ya Imam Khomeini mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kuundwa jeshi la watu milioni 20 nchini Iran.

Taasisi hiyo ya wananchi kutoka matabaka mbalimbali ya kijamii, kwa kuwa na wapiganaji wenye imani, moyo wa kujitolea na ari ya kuchapakazi imekuwa na nafasi muhimu katika matukio mbalimbali ya Mapinduzi ya Kiislamu hasa kipindi chote cha vita vya kujihami kutakatifu vya taifa la Iran dhidi ya uvamizi wa Iraq.

Jeshi la Basiji bado linashiriki katika masuala mbalimbali ya kijamii, kiutamaduni na kijeshi hapa nchini Iran. Jeshi la kujitolea la Basiji linafungamana na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

3469966

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: