IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Nusu milioni wajisajili mashindano ya Qur'ani ya Vikosi vya Basij Iran, muda waongezwa

11:23 - September 14, 2024
Habari ID: 3479433
IQNA - Muda wa mwisho wa usajili wa Toleo la 31 la Mashindano ya Qur'ani na Etrat kwa Vkosi vya  Basij vya Iran uliongezwa ambapo zaidi ya nusu milioni tayari wamejiandikisha kwa ajili ya tukio hilo.

Usajili ulianza mwishoni mwa Julai na ulipangwa kukamilika mnamo Septemba 10.

Hata hivyo, kutokana na maombi ya vituo vya Basij vya Dar-ul-Quran kote nchini, tarehe ya mwisho ya usajili iliongezwa hadi Septemba 21.

Kulingana na takwimu za hivi punde, zaidi ya washiriki 535,000 wamejisajili ambao wanahudumu katika vikosi vya kujitolea vya wananchi Iran ambavyo ni maarufu kama Basij. Baadhi pia wamejisajili pamoja na wanafamilia kushiriki katika mashidano hayo ya Qur'ani

Baada ya kukamilika kwa mchakato wa usajili, duru ya kwanza itafanyika kote nchini katika ngazi ya misikiti na vituo vya Basiji.

Kulingana na mipango hiyo, washindani wakuu katika raundi nne za kwanza watashindana katika fainali, zinazopangwa kufanyika wakati wa Wiki ya Basij mnamo Novemba.

Basij ni kikosi cha kujitolea cha kijeshi kilichoanzishwa mwaka 1979 kwa amri ya Imam Khomeini (AS), mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Aghalabu ya wanaohudumu katika kikosi hicho huwa na vijana ambao wamejitolea kuhudumia umma katika sekta mbali mbali na huwa na misimamo imara ya kidini na uaminifu kwa mfumo wa Kiislamu.

 4236279

captcha