IQNA

11:45 - November 30, 2019
News ID: 3472242
TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya 37 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yamepengwa kufanyika katika mji mtakatifu wa Mashhad mwakani.

Mkuu wa Wakfu wa Kitaifa wa Mashindano ya Qur'ani nchini Iran Bw. Karim Dolati, ameifahamisha IQNA kuwa mashindano hayo yatafanyika katika Haram ya Imam Ridha AS.

Ameongeza kuwa Taasisi ya Astan Quds Razavi (Ufawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Ridha AS) na Ofisi ya Gavana wa Mkoa wa Khorassan Razavi zitashirikiana katika kauandaa mashindano hayo.

Aidha amesema sawa na mashindano yaliyopita kutakuwa na mchujo ambapo waliotimiza masharti ndio watakaofika nchini Iran  kushiriki katika mashindano hayo.

Mwaka huu washiriki 184 wa mashindano ya Qur'ani kutoka nchi 84 walifanikiwa kufika katika nusu fainali ya mashindano ya mwaka huu.

Shirika la Wakfu la Iran huandaa mashindano ya kimatiafa ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani ya Iran kila mwaka ambapo huwa na washiriki kutoka kila kona ya dunia.

3860401

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: