IQNA

13:29 - December 09, 2019
News ID: 3472264
TEHRAN (IQNA) Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia zimetiliana saini mapatano kuhusu Ibada ya Hija katika mwa huu wa Hijria Qamaria.

Kwa mujibu wa taarifa, Ali Reza Rashidian, Mkuu wa Shirika la Hija na Ziyara la Iran akizungumza Jumapili akiwa Saudia ameashiria kuhusu kutiwa saini mapatano hayo na kusema: "Katika mazungumzo na Waziri wa Hija na Umrah wa Saudi Arabia Mohammad Saleh bin Taher Benten, tumejadili kuhusu kulinda izza, heshima, usalama na utulivu wa Mahujaji na wafanyaziyara Wairani."

Rashidian amesema kustawisha na kuimarishwa ushirikiano wa pande mbili katika kurahisisha utekelezwaji na utoaji huduma nzuri na za kiwango cha juu kwa Mahujaji kama vile uchukuzi, makazi n.k ni kati ya nukta ambazo alizijadili na Waziri wa Hija na Umrah wa Saudi Arabia.

Mkuu wa Shirika la Hija na Ziyara la Iran ameashiria matatizo waliyokumbana nayo wafanyaziyara na Mahujaji Wairani mwaka uliopita katika makazi yao mjini Madina mwaka uliopiota na kusema: "Waziri wa Hija na Umrah wa Saudia amefahamishwa kuwa, wawekezaji Wairani wako tayari kujenga hoteli bora mjini Madina."

Rashidiana aidha amesema Iran ingali inafuatilia haki za mashahidi wa Mina na kuongeza kuwa: "Nimemtaka Waziri wa Hija na Umrah w Saudia kuharakisha ufuatiliaji wa haki za mashahidi wa Mina."

Ikumbukwe kuwa wakati wa Siku Kuu ya Idul Adha mwaka 2015, maelfu ya Mahujaji wakiwemo Wairani 464 walipoteza maisha wakati wakitekeleza Ibada ya Hija katika ardhi ya Mina na maafa hayo yalijiri kutokana na usimamizi mbovu wa Saudia.

/3862709

Tags: iran ، hAJJ ، saudi arabia ، IQNA
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: