IQNA

Misri yawafuta kazi Maimamu waliojiunga na 'makundi ya kigaidi'

10:19 - December 17, 2019
Habari ID: 3472283
TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Wakfu nchini Misri imetangaza kuwafuta kazi maimamu na wahubiri saba ambao wametuhumiwa kujiunga na 'makundi ya kigaidi'.

Wizara hiyo imesema maimamu hao wote ambao ni kutoka katika mji wa Ismailia kaskazini mashariki mwa Misri wamefutwa kazi kuanzia Disemba 16 na misikiti katika eneo hilo imetakiwa kutowaruhusu maimamu waliofutwa kazi kutoa hotuba au kuswalisha sala za jamaa.

Mwezi Novemba pia, Wizara ya Wakfu Misri iliwauta kazi maimamu tisa katika maeneo ya Sohag na Qalyubiya na kuwazuia kuhutubu katika Sala  ya Ijumaa kwa tuhuma kuwa wamejiunga na 'kundi la kigaidi."

Mwezi Oktoba Chuo Kikuu cha Cairo nchini Misri kimeandaa warsha iliyojadili mada ya 'Vita Dhidi ya Ugaidi Kwa Mtazamo wa Qur'ani'.

Warsha hiyo ilifanyika Oktoba 29 katika Kitivo cha Darul Ulum cha Chuo Kikuu cha Cairo na kuhudhuriwa na waalimu pamoja na watafiti  wa Chuo Kikuu cha Al Azhar. Aidha waandishi habari kutoka vituo vya televisheni na magazeti wameshiriki katika warsha hiyo.

Lengo kuu la warsha hiyo limetajwa kuwa ni kusisitiza kuhusu haja ya kutekeleza mafundisho ya Qur'ani na kusambaza fikra za amani, uadilifu na uhuru kwa mujibu wa Qur'ani Tukufu.

3470126

captcha