IQNA

Darul Iftaa ya Misri yakosoa Washington Post kwa kumsifu kinara wa ISIS, al Baghdadi

10:24 - October 31, 2019
Habari ID: 3472195
TEHRAN (IQNA) – Taasisi ya Darul Iftaa ya Misri imelaani vikali hatua ya gazeti la Kimarekani la Washington Post kumsifu kinara wa kundi la kigaidi la ISIS (Daesh) aliyeuawa kuwa eti alikuwa 'mwanazuoni wa kidini aliyishi kwa unyenyekevu na usahali'.

Katika taarifa Idara ya Darul Iftaa ya  Kuchunguza Fatwa za Kitakfiri na Itikadi za Kufurutu Ada imesema ni kosa kubwa kwa gazeti hilo kutoa sifa kama hizo na kusisitiza kuwa gaidi aliyeuawa alikuwa mbakaji na aliwachma moto hai watu wengi na vitendo hivyo havina ufungamano wowote na Uislamu.

Darul Iftaa ya Misri imesema kumpa kinara wa ISIS sifa kama hizo kuna lengo la uuchafulia jina Uislamu, Waislamu na wanazuoni wa Kiislamu na kwamba gazeti hilo limeonysha wazi chuki zake dhidi ya Uislamu.

Taarifa hiyo imesisitiza umuhimu wa kutafautisha baina ya wanazuoni wa kweli wa Kiislamu na wale wanadia kuwa ni wanazuoni kwa malengo yao haramu.

Idara ya Darul Iftaa ya  Kuchunguza Fatwa za Kitakfiri na Itikadi za Kufurutu Ada pia imetoa wito kwa vyombo vyote vya habari kuchukua tahadhari wakati wa kufafanua kuhusu maana ya ugaidi na magaidi na kujizuia kunasibisha maovu hayo na Uislamu hasa kutokana na kuenea chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi.

Jumapili asubuhi, Oktoba 27, 2019, vyombo vya habari vya Marekani viliwanukuu maafisa wa wizara ya ulinzi ya nchi hiyo Pentagon wakidai kuwa, jeshi ISIS katika operesheni maalumu iliyoshirikisha helikopta, ndege za kivita na mapigano ya nchi kavu. Kwa mujibu wa vyombo hivyo vya habari, al Baghdadi ameuliwa na kikosi maalumu cha jeshi la Marekani katika kijiji kimoja cha mkoa wa Idlib wa kaskazini magharibi mwa Syria.

Itakumbukwa kuwa, ni Marekani hiyo hiyo ndiyo iliyomtorosha al Baghdadi kutoka jela ya Abu Ghuraib nchini Iraq mwaka 2009 na kumuandaa kwa ajili ya kuwa kiongozi wa genge la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) lililofanya jinai kubwa mno dhidi ya wananchi wa Syria na Iraq na maeneo mengine mengi duniani. Sasa hivi baada ya kuona kuwa al Baghdadi hana faida tena kwao wamejifanya kuendesha operesheni kabambe ya kumsaka na kumuangamiza gaidi huyo ili asiweze kuwafichulia walimwengu siri kubwa alizokuwa nazo kuhusu mabeberu hao.

Mara kwa mara Trump amekuwa akijigamba kuwa eti Marekani ina nia ya kweli ya kupambana na ISIS. Hata hivyo madai hayo yanakinzana kikamilifu na uhakilisia wa mambo. Inaonekana Trump amejifanya kusahau matamshi yake mwenyewe wakati wa kampeni za uchaguzi wa rais huko Marekani mwaka 2016 alipoutangazia ulimwengu kuwa serikali ya Obama ndiyo iliyoanzisha genge la kigaidi la Daesh. Wakati wa kampeni hizo za uchaguzi, Trump alisema: Obama na Hillary Clinton si watu wakweli. Wao ndio waliolianzisha genge la Daesh. Hillary Clinton na Obama ndio walioianzisha ISIS, alisema kwa kusisitiza rais huyo mwenye misimamo inayobadilika kufumba nakufumbua.

3469770

 

captcha