IQNA

18:28 - January 14, 2020
News ID: 3472371
TEHRAN (IQNA) – Kampeni mpya imezinduliwa huko mjini Dallas, Marekani kwa lengo la kuelimisha umma kuhusu misingi ya mafundisho ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kampeni hiyo maalumu imezinduliwa kwa kuwekwa bango kubwa lenye maandishi yasemayo: "Mpate Isa (Yesu) katika Qur'ani na Muhammad katika Bibilia."

Kampeni hiyo imezinduliwa na kundi moja linalojulikana kama GainPeace ambalo liko katika mji wa Chicago. Mkurugenzi Mtendaji wa GainPeace Sabeel Ahmed anasema: "Lengo letu ni 'kujenga madaraja' na kuondoa sintofahamu zilizopo. Tunataka kuwaelimisha Wamarekani wenzetu na kuwapa fursa ya kuufahamu Uislamu, kuusoma Uislamu kupitia mitandao na mabango yetu."

Amesema lengo la bango walioloezeka ni kuufahamisha Umma kuwa Nabi Isa AS si Nabii wa Wakristo pekee bali pia ni Nabii katika Uislamu. Amesema kuna dhana potovu kuwa Waislamu hawamuamini Nabii Isa AS na Bibi Maryam. "Nabii Isa ametajwa kwa mapenzi, heshima na taadhima mara 25 katika Qur'ani Tukufu naye Bibi Maryam, Mama yake Nabi Isa AS ametajwa mara 32 katika Qur'ani Tukufu,"  amesema Ahmed.

3470361

 

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: