IQNA

Awamu ya Kwanza ya Ukarabati wa Msikiti wa Mosul yamalizika

13:38 - January 22, 2020
Habari ID: 3472394
TEHRAN (IQNA) – Awamu ya kwanza ya ukarabati muhimu wa Msikiti wa Al Nouri mjini Mosul Iraq imekamilika. Msikiti huo ulihujumiwa na kubomolewa na kundi la kigaidi la ISIS (Daesh) mwaka 2017.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limetoa taarifa Jumatatu na kusema awamu muhimu ya ukarabati wa msikiti huo imekamilika ikiwa ni katika juhudi za kurejesha adhama ya msikiti huo uliojengwa karne ya 12 Miladia na ambao ulikuwa mashuhuri kutokana na mnara wake uliopinda.

Ukarabati ulianza  Oktoba mwaka jana na ujenzi wake ni sehemu ya ukarabati wa turathi za mji wa Mosul ambapo UNESCO imesema ukarabati wa turathi katika mji huo utagharimu dola milioni 100.

Kinara wa kundi la ISIS aliyeangamizwa Abu Bakr al Baghdadi alitangaza  ukhalifa wake bandia akiwa ndani ya Msikiti wa Al Nouri mwaka 2014 na magaidi wa kundi lake wakaulipia msikiti huo wa mabomu Juni 2017 wakati jeshi la Iraq lilipokuwa linakaribia kuukomboa mji wa Mosul.

Magaidi wa ISIS waliendesha kampeni ya mauaji ya kinyama nchini Iraq na Syria tokea mwaka 2014 hadi mwaka 2017 kabla ya kuangamizwa kufuatia jitihada za majeshi ya Iraq na Syria kwa ushirikiano na harakati za mapambano ya Kiislamu na washauri wa kijeshi wa Iran na Russia. Kundi hilo lenye itikadi za ukufurishaji, lilikuwa linapata himaya ya siri na ya wazi kutoka baadhi ya nchi za Magharibi, utawala wa Kizayuni wa Israel na pia baadhi ya madola ya Kiarabu hasa Saudi Arabia.

3873093

captcha