IQNA

Sayyid Hassan Nasrallah
10:48 - February 14, 2020
News ID: 3472470
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kwa kumuua kigaidi shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Qods cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Marekani ilivuka mistari yote miekundu na kwamba mauaji hayo yamegeuza mahesabu yote katika eneo la Asia Magharibi.

Sayyid Hassan Nasrallah amesema hayo jana usiku kwa njia ya televisheni kutoka Beirut, mji mkuu wa Lebanon kwa mnasaba wa arubaini ya Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na wanajihadi wenzake na kuongeza kuwa, jinai hiyo ya Washington imepelekea kufunguliwa ukurasa mpya wa historia katika eneo la Asia Magharibi.
Ameeleza bayana kuwa, "mauaji ya kamanda wa ngazi za juu wa Iran yameusaidia umma wa Kiislamu kutambua adui yao mkubwa, ambaye ni shetani mkubwa Marekani."
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amebainisha kuwa, sababu kuu ya Marekani kutekeleza mauaji hayo ya kigaidi ni kugonga mwamba malengo yake machafu katika eneo na kwamba, licha ya ugaidi huo lakini athari za Jenerali Soleimani hivi sasa zimeonekana na kuhisika zaidi kieneo na kimataifa kuliko wakati wowote ule.

Akizungumzia shakshaia ya Shahidi Qassem Soleimani aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds ch Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Sayyid Hassan Nasrullah amesema Shahidi Soleimani alikuwa na mtazamo wa kidugu kwa wapiganaji wa Jihadi wa Lebanon na kwamba mtazamo huo ulijenga uhusiano wa kidugu baina ya kamanda huyo na wapiganaji wa Hizbullah. Sayyid Nasrullah amesema: "Uhusiano kama huu ulisaidia sana kukutanisha pamoja mitazamo, mawazo, mipango, ushirikiano na jinsi ya kuvuka matatizo au hitilafu zozote zilizotazamiwa kujitokeza.” Kwa hakika mwenendo huu wa Al Haj Qassem Soleimani unathibitisha kuwa, mantiki ya Iran kuhusiana na suala la kuwepo udugu baina ya mataifa na nchi za Waislamu si nara tupu bali ni mwenendo unaotekelezwa kivitendo.

Sayyid Hassan Nasrullah anasema, kutochoka na kuwa tayafi kukabiliana na hatari za aina mbalimbali ni miongoni mwa sababu za mafanikio ya Al Haj Qassem Soleimani. Katibu Mkuu wa Hizbullah anamalizia kwa kusema: “Moja kati ya neema kubwa sana za Mweyezi Mungu kwangu mimi katika maisha yangu ni kujuana na Al Haj Qassem Soleimani na udugu na urafiki liokuwepo baina yetu, ingwa neema zote za Mwenyezi Mungu kwangu mimi ni kubwa na adhimu.”    

Katibu Mkuu wa Hizbullah amesisitiza kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haina mtazamo wa kimakundi na kimadhehebu kuhusiana na matukio ya ulimwengu na Umma wa Kiislamu na kwamba, inaamiliana na masuala hayo kwa mtazamo wa Kiislamu. Amebainisha ukweli huo kwa kusema kuwa, tangu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haikusita hata kidogo kutoa misaada ya aina mbalimbali kwa makundi na nchi za Kiislamu bila ya kujali madhehebu zao. Amesema Iran ya Kiislamu iliendelea kuisaidia Lebanon kwa hali na mali kwa ajili ya kukabiliana hujuma ya utawala haramu wa Israel licha ya kuwa katika vita vya kutwishwa vya miaka 8.

Kamanda Qassem Soleimani ambaye Januari 3 mwaka huu alielekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo aliuliwa shahidi akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha Hashd al Sha'abi na wanajihadi wengine wanane katika shambulio la kigaidi la jeshi la kigaidi la Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad.
Katika kutekeleza ahadi yake ya kulipiza kisasi kikali kwa Marekani kutokana na nchi hiyo kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na shakhsia wengine aliokuwa nao, Iran ilishambulia kwa makombora kambi ya kijeshi ya askari gaidi wa Marekani ya Ain Assad nchini Iraq hapo tarehe 8 Januari mwaka huu.

3878556

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: