IQNA

Bintiye Shahidi Soleimani: Kuuawa shahidi baba yangu kutaimarisha mapambano

14:53 - January 06, 2020
Habari ID: 3472342
TEHRAN (IQNA) -Bintiye Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani zifahamu kuwa, kuuawa shahidi baba yake kutibua mwamko mkubwa na kuimarisha harakati za mapambano au muqawama katika eneo.

Akihutubia mamilioni ya waombolezaji walioshiriki katika sala ya maiti ya baba yake na mashahidi wenzake, Zainab Soleimani ametoa onyo kali na kusema kuuawa shahidi baba yake kutaziletea Israel na Marekani madhara makubwa.
Ameongeza kuwa: "Njama ya kishetani ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kuibua mgawanyiko na hitilafu baina ya mataifa mawili ya Iran na Iraq kwa kumuua Soleimani na naibu kamanda wa Harakati ya al Hashd al Shaabi ya Iraq Abu Mahdi al Muhandis imefeli."
"Trump, wewe mraibu wa uchezaji kamari, njama yako ya kishetani ya kuibua mgawanyiko baina ya mataifa mawili ya Iraq na Iran itafeli kama ambavyo umefanya kosa la kistratijia la kuwaua Haj Qassem na Abu Mahdi ," amesema Zainab na kuongeza kuwa kitendo cha Trump kitaimarisha umoja wa kihistoria ya mataifa mawili ya Iran na Iraq ambayo yote daima yanaichukia Marekani.
"Wewe Trump mwendawazimi, wewe ni nembo ya ujinga na ni kikakragosi cha Wazayuni wa kimataifa," amesema Zainab Soleimani.
"Jinaii hii ya kinyama ya Wamarekani inaonyesha roho yao ya utendaji jinai na ubeberu hasa katika ardhi ya Palestina."

Zainab Soleimani amesema Luteni Jenerali Qassem Soleimani alikuwa na hamu kubwa ya kufa shahidi. Aidha amewahutubu maadui wa Uislamu na Iran na kusema baba yake alikuwa mpigana jihadi ambaye kutokana na hamu yake ya kufa shahidi alikuwa anafika katika mstari wa mbele kukabiliana na maadui.

Akibainisha zaidi kuhusu jihadi ya baba yake, Bi. Zainab ameendelea kusema: "Katika kipindi cha zaidi ya miaka 40, baba yangu alifanya jitihada zisizo na kikomo na alikuwa na hamu kubwa ya kufa shahidi na alipigana kwa ushujaa na maadui wa Uislamu na ubinadamu."

Aidha bintiye shahidi Soleimani amesema Wamarekani na Wazayuni wafahamu kuwa, kuuawa shahidi baba yake kumeleta mwamko mkubwa zaidi miongoni mwa walio katika mstari wa mbele wa muqawama. Aidha amesema Wazayuni na Wamarekani wafahamu kuwa  watakumbwa na mustakabali mbaya kwani nyumba zao zinashabihiana na nyumba ya buibui ambayo ni dhaifu na itaangamia tu.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, Abu Mahdi al Muhandis, Naibu wa Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq al Hashd al Shaabi pamoja na wenzao wengine wanane waliuliwa shahidi usiku wa kuamika Ijumaa tarehe tatu Januari 2020 katika shambulio la anga lililofanywa na utawala wa kigaidi wa Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad, mji mkuu wa Iraq.

3869555

captcha