IQNA

20:13 - June 15, 2020
News ID: 3472867
TEHRAN (IQNA) – Wanachama wa Jeshi la Kujitolea la Wananchi wa Iraq maarufu kama Al Hashd al Shaabi wameshiriki katika hafla ya kumuenzi shahdi Abu Mahdi al-Muhandis, naibu kamanda wa jeshi hilo aliyeuawa shahdi katika hujuma ya kigaidi ya jeshi la Marekani mwezi Januari.

Hafla hiyo imefanyika katika Makaburi ya Wadi al-Salam, Najaf Iraq, kwa mnasaba wa mwaka wa sita wa Fatwa ya Ayatullah Sayyid Ali al-Sistani kuhusu vita dhidi ya kundi la kigaidi la ISIS  au Daesh.

Ikumbukwe kuwa, tarehe 10 Juni 2014, kundi la kigaidi la Daesh liliingia na kuuteka mji wa Mosul, makao makuu ya mkoa wa Neinawa (Nineveh) nchini Iraq.

Ayatullah Sistani, mar'ja' mkuu wa Waislamu nchini Iraq katika radiamali yake ya kwanza kuhusiana na kutekwa ardhi ya nchi hiyo na magaidi alitoa fatwa ya mapambano dhidi ya magaidi hao ambapo huu ni mwaka wa sita tokea kutolewa fatwa hiyo.

Hashd as-Sha'abi imekuwa na nafasi muhimu katika kukombolewa maeneo tofaui ya Iraq kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh na daima imekuwa katika mstari wa mbele wa mapambano dhidi ya ugaidi nchini humo.

Pamoja na kuwa Hashd as-Sha'abi chini ya uongozi wa Abu Mahdi al Muhandis ilikuwa na nafasi muhimu katika kuangamiza ISIS, kamanda huyo aliuliwa kigaidi Januari 3 mwaka huu karibu na uwanja wa ndege wa ndege  wa Baghdad katika hujuma ya kigaidi ya Marekani. Al-Muhandis alikuwa ameandamana na Luteni Jenerali Qassem Solimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

3904984

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: