IQNA

Rais Hassan Rouhani
21:21 - February 16, 2020
News ID: 3472478
TEHRAN (IQNA) - Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, vikwazo vilivyowekwa dhidi ya taifa la Iran havina faida kwa maadui na kuongeza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu imevuka vikwazo vya kiwango cha juu vya Marekani.

Rais Hassan Rouhani ambaye hii leo alikuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Tehran amesema vikwazo vilivyowekwa dhidi ya taifa la Iran havikuzaa matunda yaliyotarajiwa na maadui na kuongeza kuwa, lengo kuu la mashinikizo ya kiwango cha juu ya Marekani dhidi ya serikali na taifa la Iran ni kuburuta Jamhuri ya Kiislamu kwenye meza ya mazungumzo lakini kamwe suala hilo hilo halitatatimia.

uhusuana na kadhia hii, Rais Rouhani amewaambia waandishi wa habari kwamba: "Wamarekani walikuwa wakidhani kwamba, mashinikizo ya kiwango cha juu yanaweza kuiburuta Iran kwenye meza ya mazungumzo. Hata hivyo Jamhuri ya Kiislamu imetoa kauli yake waziwazi mbele ya dunia nzima tena kwa kuweka kifua mbele, kwa uwezo na heshima na kamwe haitaburutwa kwenye meza ya mazungumzo."

Kuhusu mpango wa Amani ya Hormuz, Rais Rouhani amesema: Ni wazi kwa walimwengu wote kwamba, eneo la magharibi mwa Asia haliwezi kupata amani na utulivu bila ya kushirikishwa Iran.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia pia nafasi na mchango wa shahidi Qassem Soleimani aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika eneo la magharibi mwa Asia na kusema: Shahidi Soleimani alikuwa akifanya juhudi za kuimarisha amani katika eneo nyeti na muhimu la Ghuba ya Uajemi na magharibi mwa Asia. 

Rais Rouhani amesema: Jamhuri ya Kiislamu daima imekuwa ikitilia mkazo suala la amani na usalama wa eneo la magharibi mwa Asia na shahidi Qassem Soleimani aliyeuawa kigaidi na Marekani alikuwa miongoni mwa makamanda waliofanya jitihada kubwa kuimarisha usalama huo.

Rouhani pia ameashiria mgogoro wa Yemen na kusema: Saudi Arabia inapaswa kukomesha kabisa uvamizi na mshambulizi yake dhidi ya nchi hiyo, na masuala ya Yemene wanapaswa kuachiwa Wayemeni wenyewe. 

Sehemu nyengine ya mazungumzo ya Rais Rouhani na waandishi habari ambayo ilitawaliwa na maswali na majibu, ilihusu uchaguzi wa Bunge la Iran ulipangwa kufanyika Ijumaa ijayo.

Kuhusiana na maudhui hii Rais wa Jamhuri ya Kiislamu amejibu madai yaliyotolewa na Brian Hook anayehusika na meza ya Iran katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani aliyesema kuwa uchaguzi wa Iran ni wa kimaonyesho tu. Rais Rouhani amesema: Demokrasia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni halisi na ya kweli zaidi kuliko ile ya nchi nyingine duniani ziliwemo hata nchi za Magharibi na Marekani.

        

3879134

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: