IQNA

Dikteta wa zamani wa Misri, Husni Mubarak, ameaga dunia

17:16 - February 25, 2020
Habari ID: 3472505
TEHRAN (IQNA) -Rais wa zamani wa Misri, dikteta Hosni Mubarak amefariki dunia hospitalini jijini Cairo akiwa na miaka 91.

Mubarak amefariki Jumanne akiwa na miaka 91, wakati akiwa anapatiwa matibabu kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.

Mubarak aliitawala Misri kwa mkono wa chuma Misri kwa miaka 30, hadi pale alipopinduliwa na jeshi kufuatia maandamano makubwa ya umma mnamo mwaka 2011.

Alikamatwa mwezi Aprili, 2011 ikiwa ni miezi miwili baada ya kupinduliwa mamlakani na baadae kupatiwa matibabu kwenye hospitali za magereza na kijeshi hadi mwaka 2017, wakati alipoachiwa baada ya kusafishwa dhidi ya mashitaka yaliyokuwa yakimkabili ya kuagiza waandamanaji kuuliwa.

Mubarak alihukumiwa kifungo cha maisha jela mnamo mwaka 2012 kwa madai ya kula njama ya mauaji ya waandamanaji 239. Mahakama ya rufaa iliamuru kesi hiyo kusikilizwa upya na hatimaye mashitaka yake yalifutwa na aliachiliwa huru mwaka 2017.

Mwaka 2015 alishtakiwa sambamba na watoto wake wawili wa kiume kwa kuchepusha fedha za umma na kuzitumia kwa kuendeleza mali za kifamilia. Walihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela.

Wamisri wengi walioishi enzi ya utawala wa Mubarak wanachuhukulia wakati huo kama kipindi cha utawala wa kiimla na udikteta.

Mwaka mmoja baada ya Mubarak kupinduliwa , Mohammed Morsi mwanasiasa wa Harakati ya Ikhwanul Muslimin, alishinda uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia nchini Misri . Morsi yeye mwenyewe alitimuliwa madarakani na jeshi 2013 na kufariki 2019 akiwa jela.

Mubarak,wakati huohuo, alifungwa kifungo cha maisha kufuatia vifo vya waandamanaji 900 ambao waliuawa na vikosi vya usalama wakati wa maandamano ya 2011.

3470752

captcha