IQNA

Hofu ya kirusi cha Corona
20:47 - March 06, 2020
News ID: 3472538
TEHRAN (IQNA)- Hotuba za sala ya Ijumaa katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) leo hazikupindukia dakika 10 kufuatia amri ya Idara ya Masuala ya Kiislamu na Wakfu nchini humo.

Amri hiyo imetolewa ikiwa ni katika hatua zilizochukulia kama tahadhari kuzuia kuenea kirusi cha COVID-19 maarufu kama Corona ambacho kimeibua wahka na hofu duniani kote.

Kwa mujibu wa amri iliyotolewa na Idara ya Masuala ya Kiislamu na Wakfu ya UAE, Maimamu walitakiwa kusoma aya mbili tu za Qur'ani kisha wasome hotuba na dua iliyoandikwa na idara hiyo bila kuongeza chochote. Kwa ujumla walitakiwa wahakikishe kuwa Sala ya Ijumaa haizidi dakika 10.

Taarifa hiyo imesema hatua hiyo ilichukuliwa ili kuzuia kuenea kirisho cha Corona. Wizara ya Afya UAE imetoa wito kwa raia wa nchi hiyo kujizuia kusafiri katika nchi za kigeni na wale wanaosafiri watalazimika kukaa katika karantini kwa muda wa siku 14. Aidha siku ya Jumatano Wizara ya Elimu ya UAE ilitangaza kufungwa kwa muda wa mwezi moja shule na vyuo vikuu nchini humo. Hadi sasa watu 27 wamepatikana na kirusi cha Corona nchini UAE.

Hadi sasa zaidi ya watu 100,000 wameambukizwa kirusi cha Corona duniani huku waliofariki wakifika 3,200 wengi wakiwa nchini China.

3470836

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: