IQNA

Mwanazuoni mwandamizi wa Kiislamu alaani mauaji ya Waislamu India

16:42 - March 07, 2020
Habari ID: 3472540
TEHRAN (IQNA)- Ayatullah Nouri Hussein Hamedani ambaye ni miongoni mwa viongozi wa juu wa kidini nchini Iran amelaani ukatili na mauaji yanayoendelea kufanywa dhidi ya Waislamu nchini India na kukosoa kimya cha vyombo vya habari duniani kuhusiana na mauaji hayo.

Ayatullah Hamedani amesema kuwa, kuna habari za kusikitisha sana kuhusu hali ya Waislamu wanaodhulumiwa nchini india na suala hilo linasikitisha sana.

Amesema kuwa, linalosikitisha zaidi ni kuona ukatili huo unanyamaziwa kimya na vyombo vya habari vya kimataifa huku viongozi wa nchi za Kiislamu na jumuiya za kutetea haki za binadamu zikiendelea kutazama kwa macho tu.

Ayatullah Nouri Hamedani amesema anatarajia kwamba serikali ya India itakomesha ukatili huo mara moja na kuchukua hatua za dharura hasa kwa kutilia maanani utamaduni na historia ya wakazi wa India ya kupambana na ukoloni na ubebebru wa kimataifa, ili raia Waislamu waweze kuishi katika nchi yao kwa amani na uhuru kamili.

Vilevile amelaani vitendo vyote vya kutumia mabavu na ubaguzi wa aina zote.

Serikali ya India imefichua habari ya kuchomwa moto kikamilifu misikiti tisa na mamia ya nakala za Qur'an Tukufu katika shambulizi lililofanywa na Wahindu wenye misimamo mikali ya chuki dhidi ya Waislamu.

Gazeti la Times of India liliripoti Jumatano iliyopita kwamba, misikiti iliyochomwa moto na Wahindu wenye misimamo mikali ilikuwa misikiti mikubwa na muhimu New Delhi, mji mkuu wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa duru za kieneo, katika mashambulizi makali ya Wahindu wenye misimamo ya kigaidi kuwalenga Waislamu na yaliyodumu kwa siku kadhaa, kwa akali Waislamu 50 wameuawa na wengine mamia ya wengine wamejeruhiwa.

3883619

captcha