IQNA

Misikiti yote UAE itaendelea kufungwa kwa muda usiojulikana kutokana na corona

19:20 - April 10, 2020
Habari ID: 3472651
TEHRAN (IQNA) – Misikiti yote katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) itaendelea kufungwa kwa mauda usiojulikana ili kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19 au corona.

Vyombo vya habari nchini UAE vimesema watawala wameamua kuendelea kufunga misikiti, makanisa na maeneo mengine ya ibada nchini humo kwa muda usiojulikana ili kulinda afya wa wakazi wote.

Uamuzi huo umechukuliwa kwa pamoja na Mamlaka ya Kitaifa ya Hali ya Dharura na Kukabiliana na Maafa, Idara ya Masuala ya Kiislamu na Wakfu, mamlaka husika za afya na taasisi  mbali mbali za kidini.

Mbali na maeneo ya ibada, maeneo yote ya umma nchini UAE pia yamefungwa ikiwa ni pamoja na maduka makubwa yasiyouza vita vya dharura na maeneo ya anasa. Halikadhalika UAE, yenye wakaazi milioni 9.4,  pia imepiga marufuku safari zote za kimataifa za ndege.

Hadi kufikia Aprili 10, watu 2,990 walikuwa wameambukizwa corona nchini UAE huku wengine 14 wakiwa tayari wameshapoteza maisha.

3471091

Kishikizo: msiki Corona uae
captcha