IQNA

Misikiti ya UAE kuruhusiwa asilimia 50 ya waumini

21:53 - July 24, 2020
Habari ID: 3472993
TEHRAN (IQNA) - Kila msikiti katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) utaruhusiwa kuwa na asilimia 50 ya waumini wanaoweza kuswali ndani yake kuanzia Jumatatu Agosti 3.

Kwa mujibu wa taarifa, waumini wanapaswa kukaa umbali wa mita 50 baina yao wakiwa ndani  ya msikiti.  Tokea Julai Mosi misikiti ya nchi hiyo ilikuwa na idhini ya kuruhusu waumini wanaofika asilimia 30 ya idadi jumla ya wanaoweza kuswali. Sheria hizo zimewekwa ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19.

Swala za siku hazitazidi dakika 10, isipokuwa swala ya Magharibi ambayo muda wake uliotengwa ni dakika tano.

Aidha misaada ya kifedha kwa taasisi mbali mbali za misaada haitatolewa kwa fedha taslimu bali ni kupitia aplikesheni maalumu za simu za mkononi.

Wakati huo huo serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu imetangaza likizo ya siku nne kwa umma kwa mnasaba wa Siku Kuu ya Idul Adha ambayo itaanza Julai 30 hadi Agosti 2.

Halikadhalika kuhusu kuchinja wakati wa Idul Adha, ni watu wenye vibali rasmi tu watakaoruhusiwa kutekeleza jukumu hilo kwa kuzingatia kanuni zote za kiafya wakati huu wa janga la COVID-19.

Hadi sasa idadi ya walioambukizwa COVID-19 nchini UAE ni  zaidi ya 58,000 na walipoteza maisha ni 343.

3472065

Kishikizo: uae ، misikiti ، covid 19
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha