IQNA

Siku ya Kimataifa ya Quds

Katika Siku ya Quds, dunia yaungana kupinga utawala wa mauaji ya kimbari wa Israel

14:16 - April 05, 2024
Habari ID: 3478632
IQNA-Siku ya Quds mwaka huu 2024 imewadia huku utawala wa Kizayuni wa Israel ukiwa umekwama kwenye kinamasi cha Gaza licha ya mauaji ya kimbari unayoendelea kufanya katika eneo hilo la Palestina ambayo tokea Oktoba mwaka jana hadi sasa yamepelekea Wapalestina wasiopungua 33,000 kuuawa, wengi wakiwa ni wanawake na watoto.

Ubunifu wa Imam Ruhullah Khomeini (RA) wa kuitambulisha Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa Siku ya Quds Duniani ulikuwa ubifu wa kudumu na wa kihistoria. Baada ya miaka 45 ya ubunifu huo, Siku ya Quds Duniani inaendelea kuadhimishwa kila mwaka kwa adhama na hamasa zaidi kuliko mwaka wa kabla yake duniani kote. Katika siku hii, mwito wa kuitetea na kuiunga mkono Palestina unatolewa na watu wote wanaopigania uhuru duniani, si Waislamu pekee. Suala hili limesababisha hofu na hasira kwa utawala unaoikalia Quds kwa mabavu dhidi ya siku hii ya kimataifa.

Kwa kuzingatia hali hiyo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema katika hotuba yake ya siku ya kwanza ya mwaka mpya wa Hijria Shamsia kwamba: “Imebainika waziwazi kuwa utawala wa Kizayuni haukabiliwi tu na mgogoro wa kujilinda, bali pia uko katika mgogoro wa kujiondoa katika mgogoro huo; Umekwama kwenye kinamasi, hauwezi kujiokoa. Kuingia utawala wa Kizayuni huko Gaza kuliutumbukiza utawala huo kwenye kinamasi; Hii leo ukiondoka Gaza atakuwa umeshindwa, na ukibakia huko pia atashindwa. Hii ndiyo hali halisi ya utawala wa Kizayuni."

Hapana shaka kuwa, Ijumaa ya leo, ambayo ni ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, itakuwa moja ya siku ngumu zaidi kwa Wazayuni, kwa sababu bango kubwa la hasira na chuki ya walimwengu dhidi ya utawala huo haramu itaonekana zaidi kuliko wakati mwingine wowote katika kona zote za dunia.

3487811

Habari zinazohusiana
Kishikizo: siku ya quds ramadhani
captcha