IQNA

Harakati ya Hamas yaangusha drone ya utawala wa Israel

22:40 - April 28, 2020
Habari ID: 3472713
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imefanikiwa kuangusha ndege isiyo na rubani (drone) ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza.

Vyombo vya habari vya Palestina vimeripoti kuwa, 'drone' hiyo ya Wazayuni imetungulia na vikosi vya Hamas mashariki mwa jiji la Dir al-Balah, katika Ukanda wa Gaza na hivi sasa ipo mikononi mwa wanamuqawama hao.

Jeshi la utawala haramu wa Israel linadai kuwa ndege yake hiyo isiyo na rubani imedondoka kutokana na hitilafu za kifundi, na eti ni muhali kuvujisha taarifa zozote muhimu kutoka kwenye chombo hicho.

Vikosi vya wapigania ukombozi wa Palestina mara kwa mara vimekuwa vikitungua 'drone' za utawala bandia wa Israel, ambazo hutumiwa na utawala huo wa Kizayuni katika operesheni za mauaji na ujasusi.

Mbali na Palestina, ndege hizo zisizo na rubani za utawala haramu wa Israel zimekuwa zikiruka kinyume cha sheria katika anga za Syria na Lebanon. Utawala ghasibu wa Israel umekuwa ukitumia drone katika hujuma na mapambano ya kukabiliana na harakati za wapigania ukombozi wa Palestina.

3471283

captcha