IQNA

Vikao vya qiraa ya Qur'ani katika hospitali za Tehran Mwezi wa Ramadhani

15:05 - May 04, 2020
Habari ID: 3472734
TEHRAN (IQNA) - Vikao vya qiraa ya Qur'ani Tukufu vinafanyika katika hospitali na vituo vya tiba katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Tehran katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa Kituo cha Masuala ya Qur'ani katika Shirika la Wakfu la Iran, vikao hivyo vinfanyika kwa ushirikiano na Wizara ya Afya.
Wasomaji Qur'ani bingwa kama vile Seyed Mohsen Mousavi, Habib Mahkam, Abbas Salimi, Mehdi Gholamnejad na Mojtaba Mohammadbeigi wanashiriki katika vikao vya kusoma Qur'ani katika hospitali na vituo vya tiba.
Mpango huo wa kusoma Qur'ani unalenga kuwapa motisho wafanyakazi wa sekta ya afya ambao wako mstari wa mbele katika vita dhidi ya corona.

3471348

captcha