IQNA

Jumuiya ya Kukurubisha Madhehebu yazindua aplikesheni ya Qur’ani

19:48 - May 06, 2020
Habari ID: 3472741
TEHRAN (IQNA) – Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu imezindua aplikesheni mpya ya Qur’ani Tukufu kwa mnasaba wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu Hujjatul Islam Abdul-Hassan Ahmadi Shahrokhti amesema aplikesheni hiyo imetayarishwa kwa lugha nne ambazo ni Kifarsi, Kiingereza, Kimalay na Kiurdu.

Aplikesheni hiyo iliyopewa jina la Al-Quran Al-Kareem inajumuisha vitabu vya kielektroniki, makala, maswali na majibu ya Qur’ani Tukufu na yaliyomo katika tovuti ya alquranolkarim.com 

Hujjatul Islam Ahmadi Shahrokhti amesema aplikesheni hiyo inalenga kustawisha shughuli za Qur’ani duniani.

Aplikesheni hiyo inaweza kupatikana katika link zifuatazo:

Lugha ya Kiarabu:

https://alquranolkarim.com/android/اپلیکیشن-القرآن-الکریم/

Lugha ya Kifarsi:

 https://ar.alquranolkarim.com/android/برنامج-القرآن-الکریم/

Lugha ya Kiingereza:

https://en.alquranolkarim.com/android/quran-app/

3896799

captcha