IQNA

Muongozo

Mwanazuoni wa Al-Azhar aonya dhidi ya matoleo yaliyopotoka ya Qur'ani mtandaoni na AI

21:36 - December 31, 2024
Habari ID: 3479978
IQNA – Sheikh Abduh Al-Azhari, mwanazuoni kutoka Chuo Kikuu cha Al-Azhar nchini Misri, ameonyesha wasiwasi juu ya uwepo wa matoleo yaliyopotoka ya Qur'ani yanayopatikana kwenye mtandao au intaneti.

Sheikh Al-Azhari alionya dhidi ya kutegemea programu za Qur'ani zisizo na uhakika na akaonyesha umuhimu wa kukagua vyanzo vya majukwaa hayo kabla ya matumizi.

Aliwataka watumiaji kupakua aplikesheni au programu za Qur'ani kutoka vyanzo vinavyoaminika vilivyokubaliwa na vituo vikuu vya Kiislamu kama Al-Azhar ili kuhakikisha usahihi wa maandiko matakatifu.

“Juhudi kubwa zimefanywa katika historia kuhifadhi Qur'ani dhidi ya kupotoka, na juhudi hizi lazima ziendelee katika enzi ya kidijitali,” Sheikh Al-Azhari alisema.

Pia alionyesha hatari zinazotokana na baadhi ya programu zinazotoa maamuzi ya kidini (fatwa) yanayopingana na misingi ya Kiislamu. Sheikh Al-Azhari aliwashauri watu kutafuta fatwa kutoka kwa mamlaka rasmi za kidini, ambazo zinapatikana kwa urahisi mtandaoni.

Akizungumzia hatari za kutumia akili mnemba (AI) kwa mwongozo wa kidini, Sheikh Al-Azhari alionya dhidi ya kutegemea programu za mazungumzo zinazoendeshwa na AI kwa fatwa na taarifa za kidini.

Kutoa fatwa ni kazi maalum inayohitaji uelewa wa hali za mtu binafsi, kitu ambacho AI haiwezi kutoa ipasavyo, alisema.

3491279

Habari zinazohusiana
captcha