Katika taarifa mwenyekiti wa UMF Mohammed Moussaoui amesema Idul Fitr ambayo inatazamiwa kuwa Mei 24 nchini humo inapaswa kusherehekewa majumbani kwa sababu sheria ya kuzuia mijumuiko nchini humo inatazamiwa kuendelea hadi Juni 2.
Moussaoui , ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Ibada za Waislamu Ufaransa (CFCM) amesema kuokoa hata maisha ya mtu mmoja ni bora zaidi ya sherehe zozote za kidini.
CFCM, ambayo ni taasisi inayowakilisha maslahi ya Waislamu na Uislamu Ufaransa imtoa msaada mkubwa kwa Waislamu katika kipindi hiki cha COVID-19 nchini humo. CFCM imeweza kuishawishi serikali ya Ufaransa itenge maeneo ziada ya maziko ya Waislamu waliofariki dunia kutokana na COVID-19.
Hadi kufikia Mei 7 watu 138,000 walikuwa wameambukizwa COVID-19 nchini Ufaransa na miongoni mwao, 25,897 wamefariki dunia.