IQNA

20:17 - June 25, 2020
News ID: 3472896
TEHRAN (IQNA) – Waislamu nchini Australia wameingia na hofu ya kuenea chuki dhidi ya Uislamu baada ya ripoti mpya kubaini kuwa maambukizi mapya ya COVID-19 mjini Melbourne yalianzia katika mjumuiko wa kifamilia wa sherehe za Idul Fitr.

“Nina wasi wasi mkubwa kwani Waislamu wataanza kusakamwa , kubaguliwa na kutengwa,” amesema Adel Salman naibu mwenyekiti wa Baraza la Kiislamu la Victoria

Amesema maadui hutafuta kila kisingizio kuwahujumu Waislamu na sasa wataanza kulaumiwa kuwa hawajali maslahi ya Australia na hivyo wanaeneza kirusi cha COVID-19. 

Gazeti la Guardian la Australia limeandika ripoti kuwa maambukizi mapya ya yalianzia katika mjumuiko wa familia kubwa ya Waislamu katika mtaa wa Coburg mjini Melbourne  wakati wa shehrehe za Idul Fitr na kwamba watu wa familia hiyo walieneza COVID-19 katika maeneo ya kaskazini na kaskazini mashariki mwa mji huo.

Hadi sasa walioambukizwa COVID-19 nchini Australia ni 1,556 na waliofarikia ni 104.

3471784

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: