IQNA

Wanawake Waislamu wagawa chakula kwa wasiojiweza Australia wakati wa corona

17:23 - July 26, 2020
Habari ID: 3473001
TEHRAN (IQNA) – Makundi kadhaa ya wanawake Waislamu nchini Australia wamejitolea kugawa misaada ya chakula kwa wasiojiweza mjini Melbourne katika kipindi hiki cha janga la COVID-19 au corona.

Kila Ijumaa, wanawake wa jamiiya Waislamu mjini Melbourne hupika chakula na kukigawa kwa wale waliokumbwa na hali mbaya kutokana na zuio la COVID-19 mjini humo.

Msimamizi wa wanawake hao anasema anatumai kazi yao itabadilisha taswira potovu ya watu wengi wa Australia kuhusu wanawake Waislamu.

"Kuna dhana potovu kuhusu wanawake wanaovaa Hijabu kwamba hawatoi mchango wowote katika jamii," amesema mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Waislamu wa Victoria, Bi. Afshan Mantoo.

Anasema wanaopokea msaada wa chakula ni watu dhaifu katika jamii wakiwemo wakimbizi na wasiojiweza na miongoni mwao ni wazungu na Wahindi.

Kufuatia kuongezeka maambukiziya COVID-19, mji wa Melbourne, ambao ni  wa pili kwa idadi ya watu Australia, umeanza kutekeleza sheria kuzuia harakati za wakaazi kuanzia Julai 8.

3912723

captcha