Katika sakata hili la ubaguzi wa kidini, wanawake wa Kiislamu wamekuwa waathiriwa wakuu, wakikabiliwa na dhulma na udhalilishaji hadharani kwa sababu tu ya kuonyesha wazi imani yao kupitia hijabu.
Ripoti ya hivi karibuni kutoka SBS News imenukuu Dkt. Nora Amath, mkurugenzi mtendaji wa Islamophobia Register Australia, akisema kuwa wanawake na wasichana wa Kiislamu wanawakilisha takriban asilimia 75 ya waathiriwa wa matukio haya, huku wengi wa watekelezaji wakiwa ni wanaume wasio Waislamu. Dkt. Amath anasisitiza kuwa ingawa matukio ya kisiasa ya kimataifa yanaweza kuchochea hali hii, lugha ya kisiasa na taswira potofu kwenye vyombo vya habari vina mchango mkubwa zaidi katika kuimarisha chuki dhidi ya Uislamu.
Katika utafiti uliofanywa na vyuo vikuu vya Monash na Deakin, visa zaidi ya 600 vilivyorekodiwa kati ya Januari 2023 na Novemba 2024 vilionesha kwa wazi jinsi wanawake wa Kiislamu wanavyolengwa kwa misingi ya chuki ya kidini na kijinsia. Visa vya kushambuliwa kwa mate, kejeli za matusi, vitisho, na manyanyaso ya mtandaoni ni miongoni mwa matukio ya kawaida ambayo wanawake wanakumbana nayo wakiwa na watoto wao au wakielekea kazini.
Zaidi ya hayo, waathiriwa wengi wameripoti kuathirika kisaikolojia, wakikumbwa na hali ya mfadhaiko, wasiwasi, na kujitenga kijamii. Hii ni ishara tosha kwamba chuki dhidi ya Uislamu si jambo la kupuuzwa bali ni jinamizi linalopaswa kushughulikiwa kwa haraka, kwa ushirikiano wa serikali, vyombo vya habari, mashirika ya kijamii, na taasisi za elimu.
Tangu mwezi Oktoba 2023, utawala wa Kizayuni wa Israel ulianzisha vita vya amuaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Gaza. Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza, jeshi katili la Israeal limeua zaidi ya Wapalestina 60,000, nusu yao wakiwa wanawake na watoto. Mnamo Novemba 2024, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ilitoa hati za kukamatwa dhidi ya Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na aliyekuwa Waziri wa Vita Yoav Gallant, kwa tuhuma za jinai za kivita na jinai dhidi ya ubinadamu, ikiwemo matumizi ya njaa kama silaha ya kivita. Aidha, Israeli inakabiliwa na kesi ya mauaji ya kimbari (genocide) katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), ambapo Afrika Kusini ilifungua kesi hiyo, na mataifa 14 yakiwemo Brazil, Uhispania, Ireland, na Uturuki yameshiriki katika mchakato huo. ICJ imetoa amri kadhaa za dharura, ikiwa ni pamoja na ile ya Mei 2025 iliyoiagiza Israel kusitisha operesheni yake ya kijeshi Gaza.
3494029