IQNA

Nakala ya Kale ya Qur’ani yauzwa kwa Pauni Milioni 7 mjini London

21:50 - June 27, 2020
Habari ID: 3472904
TEHRAN (IQNA) – Nakala nadra ya kale ya Qur’ani Tukufu iliyoandikwa Iran katika karatasi ya Kichina imeuzwa kwa pauni za Uingereza milioni saba katika mnada mjini London

Nakala hii ya Qur’ani  ni ya karne ya 15 kutoka Iran wakati wa zama za utawala wa wafalme wa silsila ya Timurid na iliandikwa katika makaratasi  yenye thamani kubwa ya kichina ya zama za Ming.

Walioipiga mnada mjini katika kituo cha wapiga mnada cha Christie’s mjini London, Uingereza wameitaja nakala hiyo ya Qur’ani kuwa ya aina yake kutokana na maandishi yake ya kaligrafia yenye mistari ya samawati na dhahabu.

Kabla ya nakala hiyo ya kale ya Qur’ani kupigwa mnada ilikuwa imetabiriwa kuuzwa kuanzia pauni laki sita hadi laki tisa lakini katika manda huo wa Ijumaa ilinunuliwa kwa pauni £7,016,250. Hakuna taarifa kuhusu mnunuzi wa nakala hiyo nadra ya Qur’ani kutoka Iran.

Nakala ya Kale ya Qur’ani yauzwa ka Pauni Milioni 7

3471802

captcha