IQNA

18:07 - June 30, 2020
News ID: 3472915
TEHRAN (IQNA) –Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) umetangaza kufungua misikiti kuanzia Julai Mosi baada ya kufungwa miezi mitatu ili kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19 au corona.

Mamlaka ya Kitaifa ya Kukabiliana Majanga (NCEMA) nchini UAE imetangaza kuwa misikiti itafunguliwa lakini bado hakuna idhini ya Swala ya Ijumaa katika misikiti yote nchini humo. Aidha kila msikiti utaruhusiwa tu kuwa na asilimia 30 ya idadi yote ya watu wanaoweza kuswali humo.

Siku ya Jumatatu, msemaji wa Mamlaka ya Kitaifa ya Kukabiliana na Majanga nchini UAE Dkt. Saif Al-Dhaheri alisema aghalabu ya misikiti itafunguliwa kwa umma kwa ajili ya swala tano za kila siku lakini Swala ya Ijumaa bado haitaruhusiwa.

UAE ilitangaza kufunga maeneo yote ya ibada kuanzia Machi 16 ili kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19.

Waumini katika maeneo ya ibada yaliyofunguliwa wametakiwa kuzingatia kanunu zilizowekwa za kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19. Aidha wazee, watoto wenye umri wa miaka 12 na wale wenye magonjwa sugu wametakiwa wasifike misikitini. Halikadhlika baadhi ya misikiti itaendelea kufunguwa. Misikiti hiyo ni ile iliyo kando ya barabara, misikiti iliyo katika maeneo ya viwanda na kumbi za swala katika maduka makubwa (mall).

Hadi kufikia Juni 30, wale ambao wameambukizwa COVID-19 nchini UAE ni 48,246 na waliofariki dunia ni 314.

3471833

Tags: misikiti ، uae ، covid-19
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: