IQNA

23:03 - June 18, 2020
News ID: 3472876
TEHRAN (IQNA) – Misikiti zaidi itafunguliwa Mayalsia kwa ajili ya swala ya Ijumaa na watakashiriki katika swala watatakiwa kuzingatia sheria za kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 au corona.

Kwa mujibu wa  Baraza la Usalama wa Taifa na Wizara ya Afya,  serikali imeruhusu misikiti na surau (kumbi za kidini) kufunguliwa maadamu shheria za kuzuia kuenea COVID-19 zitazingatiwa. Kati ya masharti yaliowekwa ni kuwataka waumini watawadhe nyumbani, wafike msikitini wakiwa na mazulia ya mikeka binafsi ya kuswalia, kuzingatia kanuni za kutokaribiana na kuvaa barakoa wakati wote wakiwa msikitini. Aidha misikiti inatakiwa kuwa na vifaa vya kupima kiwango cha joto mwilini na pia kuwapa waumini huduma ya kunawa mikono kwa kutumia dawa maalumu ya kuua viruzi na halikadhalika kusajili majini ya watu wote wanaofika msikitini kwa kutumia aplikesheni maalumu ijulikanayo kama MySejahtera au daftari maalumu.

Hadi sasa walioambukizwa COVID-19 nchini Malaysia ni 8,529 na waliopoteza maisha ni 121.

3471736

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: