IQNA

Misri yatafakari kuanzisha tena swala za Ijumaa

18:59 - June 28, 2020
Habari ID: 3472908
TEHRAN (IQNA) – Waziri wa Wakfu nchini Misri Sheikh Mohammad Mokhtar Gomaa ameahidi kuwa serikali inatafakari kuhusu kuruhusu tena swala ya Ijumaa nchini humo ambayo imeendelea kupigwa marufuku hata baada ya misikiti kufunguliwa tena wiki hii.

Katika taarifa siku ya Jumapili, waziri huyo amesema anafanya mazungumzo na Kamati ya Kudhibiti Maambukizi ya Corona katika Baraa la Mawaziri ili kuomba idhini ya kuanza tena swala ya Ijumaa kwa sharti la kuzingatiwa misingi ya kiafya.

Amesema swala ya Ijumaa wiki hii itaswali tu katika Msikiti wa Sultan Hassan na watakaoshiriki ni wafanyakazi wachache wa Wizara ya Wakfu.

Siku ya Jumamosi Misri ilifungua tena misikiti kwa ajili ya swala za jamaa lakini bado hakuna idhini ya kuswali Swala ya Ijumaa.

Kwa mujibu wa masharti mapya, misikiti itafunugliwa dakika 10 kabla ya adhana na kufungwa dakika 10 baada ya swala kumalizika. Tafsiri nyingine ya sheria hiyo inasema misikiti inapaswa kufungwa nusu saa baada ya adhana.

Kwa mujibu wa sheria mpya, misikiti ambayo pamoja na makanisa iliyofunguwa kuanzia Machi, itafunguliwa tena kwa kuzingatia sheria mpya za kiafya. Kati ya sheria hizo ni kwalazimu waumini kuvaa barakoa, kuja misikiti wakiwa na zulia au msala binafsi na kushika wudhuu nyumbani au maeneo mengine lakini si msikitini. Aidha vyoo vya misikiti vitafungwa, ni misikiti mikubwa tu itakayofunguliwa na maeneo ya wanawake hayatafunguliwa. Watoto pia hawataruhusiwa kuingia misikitini.
Halikadhalika waumini wametakiwa wasikaribiane wakati wa swala na alama maalumu zimewekwa ili kuainisha sehemu ya kusimama wakati wa kuswali. 

Hadi sasa walioambukizwa COVID-19 nchini Misri ni 63,923 na waliopoteza maisha ni zaidi ya 2,708.

3907089

بازگشایی مساجد مصر بعد از سه ماه + عکس

بازگشایی مساجد مصر بعد از سه ماه + عکس

بازگشایی مساجد مصر بعد از سه ماه + فیلم و عکس

 

 

captcha