IQNA

Jeshi la Marekani lalaaniwa kwa kuhatarisha usalama wa ndege ya abiria ya Iran

17:47 - July 25, 2020
Habari ID: 3472997
TEHRAN (IQNA) – Jeshi la Marekani linaendelea kulaaniwa vikali kwa kuhatarisha usalama wa ndege ya abiria ya Iran iliyokuwa inaruka katika anga ya Syria ikielekea Lebanon.

Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imelaani vikali kitendo cha ndege za kivita za Marekani ya kutishia usalama wa ndege ya abiria ya Iran katika anga ya Syria na kuutaja uchokozi huo kuwa sawa na kigaidi.

Taarifa ya Hizbullah imelaani vikali uchokozi huo na kuitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua haraka kukabiliana na chokochoko hizo.

Waziri wa Afya wa Lebanon pia amesema kuwa uchokozi wa ndege za kivita za Marekani dhidi ya ndege ya abiria ya Iran iliyokuwa njiani kuelekea Lebanon ni uhasama wa waziwazi na kwamba ni haki ya Iran kuwasilisha mashtaka katika mahakama za kimataifa.

Harakati za mapambano ya ukombozi wa Palestina pia zimelaani kitendo hicho cha ndege za kivita za Marekani dhidi ya ndege ya abiria ya Iran na kusema kuwa kimehatarisha uhai wa raia.

Kwingineko, msemaji wa Wizara Mambo ya Nchi za Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekemea vikali hatua ya ndege mbili za kijeshi za Marekani ya kutishia usalama wa ndege ya abiria ya Iran katika anga ya Syria na kusema: Habari zaidi kuhusu tukio hilo zinafanyiwa uchunguzi na hatua za dharura za kisiasa na kisheria zitachukuliwa baada ya kukamilika uchunguzi huo.

Sayyid Abbas Mousavi amesema kuwa, baada ya tukio hilo la kihasama, mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa, Majid Takht-Ravanchi amewasiliana na Katibu Mkuu wa Umoja huo, Antonio Guterres na kusisitiza kuwa, Marekani itabebeshwa dhima na lawama za tukio lolote litakalotokea wakati ndege hiyo itakapokuwa njiani kurejea nchini.

Ujumbe huo wa Ravanchi pia umetumwa kwa balozi wa Uswisi mjini Tehran, nchi ambayo inalinda maslahi ya Marekani hapa nchini.

Naye Msaidizi wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Masuala ya Kisheria, Laya Joneydi amesema kitendo hicho cha Wamarekani kinapingana na mkataba wa safari za ndege maarufu kama Mkataba wa Chicago na kwamba ni kudharau sheria za kimataifa.

Msemaji wa kikosi cha jeshi la kigaidi la Marekani katika eneo la magharibi mwa Asia, Bill Urban, amekiri kwamba ndege za kivita za Marekani ziliifuata ndege hiyo ya abiria ya Iran lakini amedai kuwa, ni kitendo cha kiufundi kilichofanyika kwa kuzingatia vigezo vya kimataifa. Inafaa kuashiria hapa kuwa jeshi la Marekani liko nchini Syria kinyume cha sheria za kimataifa kwani serikali ya Damascus haiidhinishi uwepo huo ina inalitazama jeshi hilo la Marekani kama jeshi vamizi.

Duru za habari zinasema ndege hizo za adui zilijificha kwa makusudi nyuma ya ndege ya abiria ya Iran iliyokuwa katika anga ya Syria ili kufanya tashwishi na kuwafanya askari wa jeshi la anga la Syria waifyatulie roketi na kuitungua.

Usiku wa kuamkia Alkhamisi iliyopita ndege mbili za kivita za Marekani zilitatiza safari ya ndege ya abiria ya Iran iliyokuwa katika anga ya Syria ikielekea Beirut. Baada ya hatua hiyo hatari na ya kihasama ya ndege hizo mbili za kivita, rubani wa ndege ya abiria ya Shrika la Ndege la Mahan la Iran alipunguza kasi ya mwendo wa chombo hicho kwa ghafla, suala ambalo limesababisha majeruhi kwa baadhi ya abiria. Hatimaye ndege hiyo iliweza kutua mjini Beirut.

3472068/

captcha