IQNA

21:58 - August 03, 2020
News ID: 3473029
TEHRAN (IQNA) – Misikiti itafunguliwa tena katika mji mkubwa zaidi wa Nigeria, Lagos kuanzia Ijumaa Agosti saba lakini kwa masharti.

Misikiti kufunguliwa tena Lagos, Nigeria lakini kwa mashartiGavana wa Jimbo la Lagos, Babajide Sanwo-Olu amesema misikiti itafunguliwa tena Ijumaa Agosti saba na makanisa nayo kuanzia Jumapili Agosti 9. Amesema maeneo hayo ya ibada ni sharti yaweke sanitaza na mikono ambazo zina uwezo wa kuua virusi na pia wote watakaofika katika maeneo ya ibada wapimwe kiwango cha joto mwilini sambamba na kuzingatia sheria ya kutokaribiana.

Aidha amesema swala za kila siku hazitaruhusiwa na kwamba kwa Waislamu msikiti itafunguliwa wakati wa swala ya Ijumaa na kwa wakristo makanisa yatafunguliwa siku za jumapili.

Misikiti ilifungwa katika maeneo mengi ya Nigeria kuanzia mwezi Machi mwaka huu ili kuzuia kuenea corona.

Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni, idadi ya walioambukizwa corona nchini Nigeria ni 43,841 na waliofariki ni 888.

3914333

Tags: nigeria ، misikiti ، corona
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: