IQNA

Sayyid Hassan Nasrallah

Mripuko katika Bandari ya Beirut ni maafa kibinadamu na kitaifa

17:28 - August 08, 2020
Habari ID: 3473045
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, mlipuko uliotokea katika bandari ya Beirut ni janga kubwa la kibinadamu na kitaifa.

Mripuko katika Bandari ya Beirut ni maafa  kibinadamu na kitaifaSayyid Hassan Nasrallah alisema jana Ijumaa katika hotuba yake kuhusu hali ya sasa ya Lebanon baada ya mlipuko wa bandari ya Beirut Jumanne iliyopita kwamba mlipuko huo umegusa maeneo na matabaka yote, na hasara zake zimeyakumba maeneo yote. 

Sayyid Nasrallah amekosoa njama zinazofanywa na baadhi ya makundi na mirengo ya ndani na nje ya nchi za kutaka kuharibu jina la Hizbullah na kusema: Baadhi ya makundi ya kisiasa yametangaza kuwa mlipuko wa Beirut umetokana na maghala ya makombora ya Hizbullah lakini tunakadhibisha kwa nguvu zote madai ya kuwepo ania yoyote ya makombora au mada za milipuko za Hizbullah katika bandari ya Beirut, si katika siku zilizopita wala hivi sasa.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema kuwa, uchunguzi utaonesha kuwa hakukuweko mada za milipuko za Hizbullah katika bandari ya Beirut na lengo la madai haya ni  kulichochea taifa la Lebanon dhidi ya harakati ya Hizbullah.

Sayyid Hassan Nasrallah ameongeza kuwa, baadhi ya makundi yanataka kutumia mlipuko huo kwa malengo ya kisiasa lakini Hizbullah inaamini kuwa, hali ya sasa si wakati mwafaka wa kulipizana visasi vya kisiasa na kichama. 

Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema msimamo wa wageni kuhusiana na mlipuko wa Beirut umekuwa chanja na unatayarisha mazingira mazuri ya kuondoka Lebanon katika mzingiro na mashaka inayokabiliana nayo. 

Amesema iwapo itathibitika kwamba kuna watu waliohusika na mlipuko wa  bandari ya Beirut basi wanapaswa kuhukumiwa kiadilifu, na mwenendo kamili wa uchunguzi na kesi hiyo unapaswa kufanyika kwa uadilifu.

Maafisa wa serikali ya Lebanon tayari wameanzisha uchunguzi kuhusu mlipuko huo mkubwa uliotokea jioni ya Jumanne iliyopita katika bandari ya Beirut na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 157. Watu wengine zaidi ya elfu tano wamejeruhiwa.

Inaripotiwa kuwa moto uliotokea katika maghala ya mada za milipuko katika bandari hiyo ulisababisha mlipuko mkubwa katika maghala mengine jirani na eneo hilo yaliyokuwa na mada za Ammonium Nitrate.

3915291

captcha