IQNA

Sheikh Taruti kuongoza Baraza Kuu la Kimataifa ya Kuhifadhi Qur’ani

19:25 - September 27, 2020
Habari ID: 3473208
TEHRAN (IQNA) – Qarii mashuhuri wa Qur’ani Tukufu nchini Misri Sheikh Abdul Fattah Taruti ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kimataifa la Kuhifadhi Qur’ani.

Kwa mujibu wa tovuti ya youm7, Jumuiya ya Kimataifa ya Waislamu (MWL),  imemteua Sheikh Taruti kuongoza  baraza hilo.

Taruti alizwaliwa mwaka 1965 katika kijiji cha Tarut karibu na mji wa Zagazig jimboni Sharqia. Alianza kuhifadhi Qur’ani akiwa na umri wa miaka mitatu na alifanikiwa kuhifadhi Qur’ani kikamilifu akiwa na umri wa miaka 8. Taruti alisoma katika tawi la Zagazig la Chuo Kikuu cha Al Azhar na aliendelea  kuimarisha uwezo wake wa Qur’ani kwa kupata mafunzo kwa kutoka kwa wasomi wakubwa kama vile Sheikh Mohammad Al-Lithi, Shahat Anwar and Saeed Abdul Samad.

3925686

captcha